Wednesday, July 10, 2013

NHC YAMPIGA TAFU MISS TANZANIA 2012 KUJENGA BWENI LA ALBINO BUHANGIJA

Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (kulia) akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 4.1 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Susan Omari jijini Dar es Salaam jana. Fedha hizo ni kwaajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) linalojengwa katika shule ya Msingi Buhangija mkoani Shinyanga. Fedha hizo ni maalum kwaajili ya kununulia mabati ya kuezekea bweni hilo. Kwa mujibu wa Brigitte zaidi ya Shilingi milioni 60 zinahitajika kukamilisha ujenzi huo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...