Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Kampuni ya Andoya Hydroelectric Company katika kijiji cha Lifakara wilayani Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Menas Andoya
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa kupeleka umeme Mbambabay katika wilaya mpya ya Nyasa kutoka kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013. Kulia ni Mkewe Tunu na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabiti Mwambungu. Watatu Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiendesha pikipiki wakati alipozindua Mradi wa Pikipiki wa Kikundi cha SACCOS ya vijana wa Mbinga kwenye uwanja wa CCM mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapongeza baadhi ya waendesha pikipiki wa Mbinga baada ya kuzindua mradi wa pikipiki za kikundi cha SACCOS ya vijana wa Mbinga kwenye uwanja wa Mpira wa CCM mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakizungumza na Mzee Andrea Mapunda (84) wakati alipotembelea shamaba la kahawa la mzee huyo katika kijiji cha Masumuni wilayani Mbinga wakiwa katika ziar ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
No comments:
Post a Comment