Tuesday, July 02, 2013

Rais Wa Marekani Barack Obama akiwasili Nchini Tanzania


 
Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Obama wakitembea kwa pamoja
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Michelle  Obama muda mfupi baada ya kuwasili kwa Rais Obama nchini kwa ziara ya siku mbili nchin.
 Mhe. Rais Obama akiongozana na Mkuu wa Majeshi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange  mara baada ya kukagua gwaride la heshima.
Mhe. Rais Obama akikagua Gwaride la Heshima
 Mhe. Rais Obama na Mhe. Rais Kikwete wakisikiliza nyimbo za Mataifa yao zilizopigwa kwa Heshima ya Rais Obama.
 Mhe. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, Mama Michelle Obama  na Viongozi wengine wa Serikali wakiwa Uwanjani hapo wakati wa mapokezi.
Mhe. Rais Obama akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mkewe Mhe. Mama Salma Kikwete na Mama Michelle mara baada ya kupokelewa.
 Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.nyuma ya Rais na mgeni wake ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya Rais huyo wa Marekani  kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Padu Ameir Kificho katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo mchana.Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Freddy Maro-IKULU

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...