MREMBO atakayetwaa taji la Redds Miss Temeke 2013,
linalofanyika Ijumaa Julai 5, mwaka huu ataondoka na zawadi za jumla ya Sh.
Milioni 3,250,000 ikiwa ni zawadi kubwa zaidi kutolewa katika mashindano yote
ya urembo, yaliyofanyika mwaka huu.
Mshindi huyo, atapata ofa ya mwaka mzima kutoka RIO
gym & Spa, iliyopo Quality Center, kutumia vifaa vyote ndani ya gym hiyo
ambayo gharama yake ni Milioni 1,400,000, pia atajinyakulia simu ya kiganjani
yenye thamani ya Sh 700,000 , dinner set kutoka AKO Catering yenye thamani ya
Sh,150,000 sanjari na pesa taslim Sh. Milioni 1, hiyo jumla yake ni Milioni
3,250,000.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ambayo mgeni
rasmi atakuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abas Mtemvu atajinyakulia kitita cha
Sh.800,000 pesa taslim na dinner set ambayo thamani yake ilikuwa bado
haijathibitishwa na mdhamni wa zawadi hiyo wakati mshindi wa tatu ambao wote
kwa pamoja ni wawakilishi wa Miss Temeke, yeye atajipatia fedha taslimu Sh
700,000.
Sh , 400,000 zitakwenda kwa mshindi wa nne na
atakayeshika nafasi ya tano yeye ataibuka na Sh 300,000. Washiriki wengine
ambao hawatabahatika kuingia katika nafasi ya tano bora, wote watapewa
Sh,200,000 kwa maana ya kifuta jasho. Tumelenga zawadi za fedha zaidi, hii ni
kutokana na ugumu wa maandalizi kwa warembo ambao hugharamika zaidi, kiasi nasi
kuona kuna kila namna ya kuwapunguzia maamivu hayo.
Shindano hilo, linatarajiwa kuwa na burudani ya
kipekee kutoka kwa mshindi wa tungo bora ya Bongo Fleva ya Kili Music mwaka
huu, Ben Paul sanjari na Twanga Pepeta ambayo mwishoni mwa wiki, ilizindua
albamu yake ya 13 kwa mafanikio makubwa.
Warembo watakaopanda jukwaani Julai 5 ni kutoka
Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambao wanawania taji linaloshikiliwa na Miss
Tanzania namba tatu, Edda Sylvester walikuwa chini ya wakufunzi Suzy Mwenda na
Shadya Mohamed wakati kwenye kucheza nako walikuwa na walimu wawili Super
Bokilo na Charles.
Warembo hao ni pamoja na Axsaritha Vedastus, Darling
Mmary, Esther Muswa, Hyness Oscar, Irene
Rajab, Jamila Thomas, Latifa Mohamed, Margreth Gerald, Margreth Olotu, Mey
Karume, Mutesi George, Naima Ramadhan, Narietha Boniface , Stella Mngazija na
Svtlona Nyameyo .
Shindano hilo limedhaminiwa na kinywaji cha Redd's,
Dodoma Wine, Gazeti la Jambo Leo, Cloud’s Media, Blogu ya Wananchi (Le Mutuz),
Fredito Entertainment, CXC Africa tours & Safaris, RIO Gym & Spa, 100.5
Times FM na Kitwe General Traders. Mbali ya wadhamini hao pia Redds Miss Temeke
imechangiwa katika ufanikishaji na Mbunge wa Jimbo hilo, Abbas Mtemvu na
mwanamichezo maarufu nchini Geofrey Nyange Kaburu hasa kwa upande wa zawadi.
Temeke, imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma
waliopata mafanikio katika mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa
kupata uzoefu wa kujiamini katika njanja mbalimbali. Miongoni mwao ni Miriam
Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika fainali za mitindo
zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa Elite Model Look, baadaye
kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss Earth World, zilizofanyika China.
Pia, Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001),
na kutwaa taji la Miss Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya
mitindo katika nchi za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla.
2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo
na Irene Uwoya.
Jokate alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia
kushika nafasi ya pili Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's
na gazeti la Citizen. Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika
nafasi ya nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010
alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
Nafasi nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na
warembo kutoka Temeke ni pamoja na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania
mwaka 2000, Regina Mosha mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey
mshindi wa pili Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na
Edda Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds
Miss Temeke.
BMP Promotions inayoandaa mashindano haya kwa mwaka
wa 18 sasa, inatanguliza shukrani zake wadhamini wetu kwa miaka hiyo, sanjari
na vyombo vyote vya habari kwa ujumla wake, kwani ndio waliofanikisha kuandaa
Miss Temeke kwa ufanisi katika muda wote huo, shukrani sana.
Benny Kisaka
Mkurugenzi BMP Promotions
No comments:
Post a Comment