Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) inayoongozwa na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara, pamoja na Menejimenti ya TANAPA, leo Januari 31, 2025, inashiriki hafla ya utoaji wa Tuzo za The Serengeti Awards inayofanyika katika Hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha.
Tuzo hizo zinalenga kutambua na kuthamini mchango wa wadau wa uhifadhi na utalii katika kukuza sekta ya uhifadhi na utalii pamoja na kuitangaza Tanzania kupitia vivutio vyake mbalimbali vya utalii.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, huku tukio hilo likihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, pamoja na wadau wa sekta ya utalii.









No comments:
Post a Comment