Tuesday, March 17, 2009

Papa Benedicto aanza ziara ya Afrika


Papa Benedict XVI akipanda ngazi kuelekea katika ndege yake maalum kwenye uwanja wa ndege wa Fiumincino, Roma kwa ajili ya kuanza safari yake katika ziara ya siku sita barani Afrika jana asubuhi. Atatembelea nchi za Cameroon na Angola.

Reuters
VATICAN, Italy

KIONGOZI mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Benedict XVI ameanza ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu alipokabidhiwa wadhifa huo, huku akieleza kuwa suala la usambazaji wa kondomu si jibu sahihi dhidi ya Ukimwi.

Akiwa njiani kuelekea nchini Cameroon, sehemu ya kwanza katika ziara yake hiyo ya siku sita kwa Afrika, Papa Benedict alisema kuwa kanisa lake litaendelea kusimama mstari wa mbele kupambana dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa Afrika kwa kutumia misingi ya wazi ya kitabu kitakatifu cha Biblia.

Ziara hiyo ya Papa ni ya kwanza kwa Afrika tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo ya juu kwa kanisa Katoliki duniani miaka minne iliyopita, huku akieleza kuwa “hakuna uwezekana wa kutokomeza maambukizi ya ukimwi kwa kuhamasisha matumizi ya kondom, zaidi kwa kufanya hivyo ni kuongeza ukubwa wa tatizo,” alisema wakati akiwa kwenye ndege yake mara baada ya kuanza safari kuelekea Cameroon.

Kama hakutatokea mabadiliko katika ziara yake hiyo, Papa atatumia siku sita za ziara yake katika nchi za Cameroon na Angola, huku taarifa zikieleza kuwa hali katika mji mkuu wa Cameroon, Younde, ulio kituo cha kwanza cha Papa uko katika tahadhari ya hali ya juu.

1 comment:

boniphace said...

Karibu Pope Benedict; umekuja kipindi kizuri cha Kwaresma lakini ziara hii umefanya kwa nchi chache mno hali ambayo inatufanya kujiuliza kiasi maana Afrika ni kubwa na siku zinavyoenda imani inapungua. Nakubaliana nawe katika hilo la mipira!

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...