Sunday, March 01, 2009

Ohhooo Dawasco hawana utani



SHIRIKA la usambazaji maji safi jijini Dar es Salaam (DAWASCO), limesema kuanzia sasa litakata maji kwa maeneo badala ya mtu mmoja mmoja, kama hatua ya kushiniza wateja wake kulipa malimbikizo ya ankara zao za maji.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za shirika hilo jana, Afisa Mkuu wa Biashara wa shirika hilo Raymond Mndolwa, alisema wanatoa siku saba kwa wateja waliolimbikiza Ankara za maji kulipa madeni yao.

“Tunatoa siku saba kwa wadaiwa sugu wa DAWASCO kulipa Ankara zetu kuanzia leo tarehe 1 (jana). Wale wote ambao hawatalipa tutakata maji katika maeneo yao," alisema Mndolwa.

Alifafanua kwamba Dawasco itafanya hivyo kuepuka usumbufu unaowakumba kwa kuwa wateja wake wanapokatiwa maji huwaita vishoka na kuwatumia kuwaunganishia maji na kulitia hasara shirika.

Alitaja maeneo sugu yenye wateja wengi wanaodaiwa na shirika hilo na ambayo yataathirika na zoezi hilo iwapo wateja wake hawatalipa madeni yao ndani ya siku saba kuwa ni Sinza A na B, Mikocheni, Masaki, Kijitonyama na Makongo juu. Habari hii ya Fred Azzah wa Mwananchi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...