Wednesday, March 18, 2009

Malya afungwa miaka mitatu

Deus Mallya aliyedaiwa kuwa dereva wa Marehemu Chacha wangwe, Mbunge wa Tarime aliyekufa katika ajali njiani akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam, amehukumiwa mvua tatu jela (miaka mitatu) na Hakimu Mkazi wa Dodoma.
Mallya amekutwa na hatia ya kuendesha gari bila leseni na kusababisha kifo cha Mbunge huyo.
Wakili aliyekuwa anamtetea, Godfrey Wasonga alijikuta akitokwa na machozi baada ya mahakama kutamka kuwa imemtia hatiani kwenye mahakama hiyo ambayo ilifurika watu wengi waliofika kusikiliza hukumu hiyo.
Hakimu Mkazi, Thomas Simba alisema kuwa mahakama imeridhika pasipo na shaka kuwa kijana huyo ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo na kwamba kifo cha marehemu kilitokana na mwendo kasi.
Baada ya hakimu kusoma maelezo hayo wakili wa mshitakiwa Godfrey Wasonga alianza kulia hali iliyoonyesha kuwa alikwisha ona mwelekeo wa kesi hiyo unamuendea vibaya mteja wake.
Hakimu alisema kuwa kutokana na sheria ya makosa ya usalama barabarani iliyofanyiwa marekebisho na bunge mwaka 2002 namba 63 kifungu cha pili kifungu kidogo (a) inasema kuwa kutokana na makosa yanayofanana na makosa ya mtuhumiwa, adhabu yake inaanzia miaka mitatu na kuendelea.
Hakimu huyo alisema kuwa kutokana na utetezi wa mshitakiwa ameamua kumfunga miaka mitatu kwa kosa la kuendesha gari mwendo kasi na kusababisha ajali.
Aliendelea kusema kuwa kwa kosa la kuendesha gari bila ya kuwa na leseni mahakama inamhukumu kwenda jela mwaka mmoja lakini akasemakuwa adhabu hizo zinakwenda pamoja, hivyo atatumikia kifungo cha miakamitatu gerezani.
Alisema kuwa kifo cha Wangwe kilisababishwa na mlango wa kushotoambao ulimbana na kufafanua kuwa ushahidi ulithibitisha kuwa marehemu hakuwa analiendesha gari hilo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...