Monday, March 30, 2009

mzee wa vijisenti kizimbani

Taarifa zilizotufikia hivi karibuni zinasema kuwa mzee wa vijisenti na Waziri wa zamani wa Miundombinu bwana John Chenge amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kinondoni na kusomewa mashitaka matatu ya kusababisha vifo vya watu watatu.

Alitinga mahakamani hapo akiwa ametilia viwalo vyake kama kawaida huku akitoa tabasamu kama ilivyo kawaida yake huku akisubiriwa na watu kibao, huku wengine wakionekana kuwa na shauku ya kutaka kumwona 'live' na wengine wakipiga vikelele kelele vidogo wakisema muzee wa vijisenti.

Yeye mwenye alionekana kuwa kawaida tu. Aliwasili na gari jingine VX na akaondoka na gari jingine. Kwa jinsi watu walivyokuwa kibaoi ilibidi apitie mlango wa nyuma na tena wa mahakama ya mwanzo ya kinondoni na kupuruchuka zake tim. Amejidhamini mwenye kwa kiasi cha Sh milioni moja. Kesi itatajwa tena siku itakayotajwa baadaye.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...