Monday, March 23, 2009

Hoteli za kitalii Paradise na Oceanic bay zateketea kwa moto




HOTELI  za Paradise Holiday Resort na Oceanic Bay Hotel zenye hadhi ya nyota tatu jana ziliteketea kwa moto na kusababisha hasara ya mali ya zaidi ya shilingi bilioni 20 huku kukiwa hakuna taarifa ya watu waliojeruhiwa  katika tukio hilo.

Watu walioshuhudia tukio hilo walisema chanzo cha moto huo ulioanza kuwaka saa 4.38 asubuhi, ni hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye jiko la hoteli ya Paradise na kusababisha cheche za moto zilizoruka na kukamata paa la jiko hilo  kisha kusambaa kwenye maeneo yote ya hoteli hiyo na baadaye moto huo kuhamia kwenye hoteli jirani ya Oceanic Bay.

Mashuhuda hao ambao wengi wao ni wafanyakazi wa hoteli hizo mbili walisema jitihada za awali za kuudhibiti moto zilishindikana kutokana moto huo kusambaaa kwa kasi kubwa kulikochangiwa na upepo mkali wa bahari ya  hindi ambapo hoteli hizo zote zimejengwa pembezoni mwa fukwe hizo huku zikiezekwa kwa paa la makuti.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...