Sunday, March 22, 2009

Juma Nature atoka kivyake





MSANII Juma Nature ambaye jana usiku alikuwa akizindua albamu yake ya ‘Tugawane Umasikini’ na Sauti na vyombo ya Ferouz Shaban alijaza umati mkubwa wa watu kiasi cha wengine kukosa pa kusimama. Kiujumla watu walikuwa kibao lakini kitu kimoja noma ilikuwa kwamba uzinduzi huo ulitawaliwa na harufu ya bangi katika ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya vijana kuamua kugawana bangi katika uzinduzi huo uliofanyika Jumamosi usiku.

Usiku huo ulio hudhuriwa na waheshimiwa wabunge kutoka jimbo la Temeke, Abass Mtevu na Mbunge viti Maalumu, Al-Shymaa Kwegyir ambaye aliposimama jukwaani kusalimia alishangiliwa na vijana waliyojaa ukumbimni baada ya kuwataka kupiga vita mataumizi ya viungo vya watu wenye ualemavu wa ngozo kwa imani ya kujiongezea utajiri.

Usiku huo ulitawaliwa zaidi na vijana wa umri kati ya mika 15 hadi 30 hivi kwani hukukuwa na watu wa umri mkubwa ukiacha waheshiwa ambao walikuwa wamekaa na mwanamasumbwi maarufua Mbwana Matumla aliyeambatana na mkwe kwenye meza maalumu.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...