Sunday, March 22, 2009

Kwembe kumenuka




MDAU kutoka Kwembe ametuambia kwamba wakazi wa Kwembe Kati, Dar es Salaam wamewazuia Maofisa Ardhi kupima viwanja katika eneo lao baada ya polisi zaidi ya 20 kutawanywa katika eneo lao ili wasimamie upimaji huo badala ya kutumia kamati ya wananchi kama walivyokubaliana.

Awali wakazi hao waliwazuia watendaji hao kupima viwanja hivyo vilivyo katika mradi wa viwanja 600 juzi kwa kile walichodai kutumia polisi kulazimisha upimaji badala ya kuishirikisha kamati ya wakazi kama ilivyokubaliwa katika kikao cha pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya, Fabian Massawe, kamati na maofisa ardhi hao hivi karibuni.

Pia wakazi hao takriban 300 waliyo katika mradi huo kupitia kamati yao ya watu 10 walikubaliana na uongozi wa wilaya kupitia upya mapendekezo ambayo yanahusu fidia kwa wale ambao miundombinu kama barabara, zinapita katika maeneo yao na wenye hati tayari baada ya kuonekana wanapata viwanja vidogo kuliko makubaliano.

“Tulipeleka mapendekezo kumi ambayo yalipaswa kutolewa majibu kabla maofisa hawa hawajaja kuendelea kupima, tulitaka ufafanuzi kuhusu ramani inayotumika na namna ambavyo mipaka ya mawe inawekwa juu ya mipaka mingine, tulitaka hayo yarekebishwe lakini tunashangaa wanakuja na polisi,” alisema Jackton Manyerere mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

“Tunampataka Kanuti (jina la kwanza ni Dioscory Kanuti-Ofisa Mipango Ardhi) atufafanulie ramani ipi inatumika maana tangu mwanzo tupo nae katika vikao na Mkuu wa Wilaya, kwa nini anatuchanganya hivi,” alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hilda Mushi ambaye ramani ya awali ilionyesha barabara inapita katikati ya nyumba yake.

Hata hivyo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Upimaji Milki Mijini, Saimon Katambi baada ya kuangalia ramani iliyokuwa inatumika, aligundua kuwa haikuwa ramani inayopaswa kutumika na ndipo alipotoa ramani halali ambapo Ndaki alipoagiza upimaji uendelee kwa ramani sahihi.

Sakata hilo lililodumu zaidi ya saa tisa, liliishia kwa wakazi hao kuwataka maofisa ardhi kukaa pamoja na kamati, Mkuu wa Wilaya na Waziri mwenye dhamana, John Chiligati, kupitia mapendekezo ya wananchi ili upiamji uendelee.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...