Monday, March 02, 2009

Mramba, Yona kusomewa maelezo leo



MAELEZO ya awali kuhusu kesi ya kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh 11 bilioni, inayowakabili mawaziri wawili wa zamani na katibu mkuu wao, yanatarajiwa kusoma

Mawaziri wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Basil Mramba, Daniel Yona na Katibu mstaafu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.


Leo washitakiwa hao watasomewa maelezo ya awali kuhusu kesi yao, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mara ya mwisho kesi hiyo ilipotajwa Februari 2 mwaka huu, upande wa mashitaka ulisema upelelezi umekamilika.

Washitakiwa hao, wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh 11 bilioni.

Wanadaiwa kuwa wakiwa waajiriwa wa serikali walitumia madaraka yao vibaya na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya M/S Alex Stewart ya nchini Uingereza kinyume na ushauri uliotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Habari imendikwa na Nora Damian.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...