Tuesday, March 31, 2009

JWTZ kupeleka kikosi Darfur



BATALIANI mbili za Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vinatarajiwa kuondoka nchini Juni mwaka huu kuelekea katika eneo Darfur, Sudan kujiunga na vikosi vingine vya askari wa Umoja wa Mataifa (UN), kulinda amani katika eneo hilo.

Waziri wa ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dokta Hussein Mwinyi alisema hayo jana alipozungumza na Mwananchi kuhusu askari hao wa JWTZ kujiunga katika ulinzi wa amani Darfur.


Dk. Mwinyi alisema batalian hizo mbili jana zilielezwa hali halisi ya sasa ya eneo la Darfur na Dk. Salim Ahmed Salim katika eneo la Msata.

“Askari wetu wataondoka Juni kwenda Darfur, Sudan, kujiunga na wenzao wa mataifa mengine katika kazi ya kulinda amani eneo hilo,”

“Dk. Salim amezungumza na vikosi vya askari wetu wa kulinda amani na leo (jana) na kuwaeleza hali halisi ya eneo hilo kwa sasa, na si kuwaaga,” alisema

Alisema vikosi hivyo vinafanya mazoezi katika eneo hilo wakati wakisubiri serikali kukamilisha baadhi ya vifaa kabla ya kuondoka.

Alifafanua kuwa vikosi hivyo vya Tanzania vyenye askari 600 na 800 wa miguu vitaungana na vikosi vya nchi nyingine ambavyo tayari vipo Darfur.

Kuhusu Somalia waziri huyo wa ulinzi alisema kuwa JWTZ itatoa mafunzo kwa vikosi vya askari wan chi zitakazofanya kazi ya kulinda amani nchini humo. 


No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...