Tuesday, March 31, 2009
JWTZ kupeleka kikosi Darfur
BATALIANI mbili za Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vinatarajiwa kuondoka nchini Juni mwaka huu kuelekea katika eneo Darfur, Sudan kujiunga na vikosi vingine vya askari wa Umoja wa Mataifa (UN), kulinda amani katika eneo hilo.
Waziri wa ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dokta Hussein Mwinyi alisema hayo jana alipozungumza na Mwananchi kuhusu askari hao wa JWTZ kujiunga katika ulinzi wa amani Darfur.
Dk. Mwinyi alisema batalian hizo mbili jana zilielezwa hali halisi ya sasa ya eneo la Darfur na Dk. Salim Ahmed Salim katika eneo la Msata.
“Askari wetu wataondoka Juni kwenda Darfur, Sudan, kujiunga na wenzao wa mataifa mengine katika kazi ya kulinda amani eneo hilo,”
“Dk. Salim amezungumza na vikosi vya askari wetu wa kulinda amani na leo (jana) na kuwaeleza hali halisi ya eneo hilo kwa sasa, na si kuwaaga,” alisema
Alisema vikosi hivyo vinafanya mazoezi katika eneo hilo wakati wakisubiri serikali kukamilisha baadhi ya vifaa kabla ya kuondoka.
Alifafanua kuwa vikosi hivyo vya Tanzania vyenye askari 600 na 800 wa miguu vitaungana na vikosi vya nchi nyingine ambavyo tayari vipo Darfur.
Kuhusu Somalia waziri huyo wa ulinzi alisema kuwa JWTZ itatoa mafunzo kwa vikosi vya askari wan chi zitakazofanya kazi ya kulinda amani nchini humo.
Monday, March 30, 2009
mzee wa vijisenti kizimbani
Taarifa zilizotufikia hivi karibuni zinasema kuwa mzee wa vijisenti na Waziri wa zamani wa Miundombinu bwana John Chenge amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kinondoni na kusomewa mashitaka matatu ya kusababisha vifo vya watu watatu.
Alitinga mahakamani hapo akiwa ametilia viwalo vyake kama kawaida huku akitoa tabasamu kama ilivyo kawaida yake huku akisubiriwa na watu kibao, huku wengine wakionekana kuwa na shauku ya kutaka kumwona 'live' na wengine wakipiga vikelele kelele vidogo wakisema muzee wa vijisenti.
Yeye mwenye alionekana kuwa kawaida tu. Aliwasili na gari jingine VX na akaondoka na gari jingine. Kwa jinsi watu walivyokuwa kibaoi ilibidi apitie mlango wa nyuma na tena wa mahakama ya mwanzo ya kinondoni na kupuruchuka zake tim. Amejidhamini mwenye kwa kiasi cha Sh milioni moja. Kesi itatajwa tena siku itakayotajwa baadaye.
Alitinga mahakamani hapo akiwa ametilia viwalo vyake kama kawaida huku akitoa tabasamu kama ilivyo kawaida yake huku akisubiriwa na watu kibao, huku wengine wakionekana kuwa na shauku ya kutaka kumwona 'live' na wengine wakipiga vikelele kelele vidogo wakisema muzee wa vijisenti.
Yeye mwenye alionekana kuwa kawaida tu. Aliwasili na gari jingine VX na akaondoka na gari jingine. Kwa jinsi watu walivyokuwa kibaoi ilibidi apitie mlango wa nyuma na tena wa mahakama ya mwanzo ya kinondoni na kupuruchuka zake tim. Amejidhamini mwenye kwa kiasi cha Sh milioni moja. Kesi itatajwa tena siku itakayotajwa baadaye.
GOVERNOR GENERAL wa Australia awasili nchini
GOVERNOR GENERAL wa Australia Mhe. Quentin Bryce akisalimiana na wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius nyerere alipowasili Nchini leo jioni kwa ajili ya kuanza ziara ya siku tatu ya kiserikali hapa Nchini. Kushoto Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein.
Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mgeni wake GOVERNOR GENERAL wa Australia Mhe. Quentin Bryce alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo kwa ajili ya kuanza ziara ya siku tatu ya kiserikali hapa Nchini. Picha hizi ni za Amour Nassor (VPO)
Vodacom regatta mbio za mashua
Machimbo ya kunduchi kibano mtindo mmoja
Mambo si mambo katika machimbo ya Kunduchi ambapo kichapo kimekuwa kikitembea mara kwa mara wachimbaji wametimuka na wengine kudinda kutoka lakini hivi sasa ulinzi mkali umeimarishwa katika machimbo hayo ili kuwazuia wachimbaji wasio na leseni wasiweze kuendelea kuchimba mahali hapo kwa kuwa wanaharibu mazingira.
Kuimarishwa huko kunatokana na utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete la hivi karibuni la kuzitaka mamlaka husika kuwazuia wachimbaji hao na kuwachukulia hatua kali wale watakaokaidi agizo la kuondoka mahali hapo.
Katika taarifa yake, Rais Kikwete alizitaka Manispaa ya jiji kwa kushirikiana na Kinondoni kuwaondoa wachimbaji hao na kumtaka Kamishna wa madini kusimamia zoezi zima la kuwaondoa wachimbaji hao.
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo hilo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Karunguyeye alisema kuwa zoezi hilo litakuwa la kudumu mpaka wananchi hao watakapoacha kuchimba kokoto katika eneo hilo.
Sunday, March 29, 2009
Ajali mbaya ya treni yaua watu sita
HABARI zilizotufikia katika deski letu la Mzee wa Mshitu zinasema kuwa watu sita wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa kufuatia treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana na treni ya mizigo Mpwapwa mkoani Dodoma jana.
Ajali hiyo ilisababisha mabehewa kadhaa ya terni hizo kuanguka huku baadhi ikiwemo lililobeba abiria kuharibika vibaya na kulazimu wataalam kutafutwa ili kulikata na kuokoa watu walio wazima au maiti ndani ya behewa hilo.
Mwananchi imefika eneo la ajali na kujionea hali halisi ikiwemo kushuhudia shughuli ya ukataji behewa hilo lenye abiria ndani ikifanyika kwa kusuasua kutokana na uduni wa vifaa vinavyotumiwa na mafundi wa Kampuni ya Reli (TRL) wakishirikiana na jeshi la polisi.
Hata hivyo hadi majira ya saa 10:15 jana maiti tano za abiria wote wakiwa wanaume zilikuwa zimeokolewa katika ajali hiyo, ambapo majeruhi walipekewa katika hospitali ya Mpwapwa kwa matibabu. Picha za mdau Faraja Jube.
MWANZA YAWAMIWA na MITINDO MOTO MOTO
Kwa Mara Ya Kwanza Mwanza na Wakazi wake watashuhudia Mitindo Moto Moto Kutoka Mbunifu gwiji Kutoka Dar es Salaam…Mustafa Hassanali Siku ya Jumamosi Tarehe 4 Aprili Katika Ukumbi wa NEW MWANZA HOTEL Saa Mbili Usiku.
MAONYESHO haya yatakayojulikana kama “SATOLICIOUS” pia Yataonyesha Kipaji Cha Mbunifu Maarufu Kutoka Mwanza Chris Designer ambaye ataonyeshwa na Wanamitindo Maarufu Kutoka DAR ES SALAAM na MWANZA.
KIINGILIO itakuwa VIP 20,000 na Vya Kawaida 10,000 TU…Usikose Show hiyo ya kukata na shoka ….Tiketi Zinapatikana New Mwanza Hotel au PIGA NAMBA 0784303880
Maonyesho Haya Yamedhaminiwa na ZAIN...Ulimwengu Maridhawa, Coca-Cola na NYANZA ROAD WORKS.
Mustafa Hassanali ni mbunifu maarufu aliyebobea. Kazi zake ni za ubunifu wa hali ya juu, nakshi ya aina ya kipekee ambayo haina upinzani katika dunia ya mavazi na mitindo hapa Tanzania.
Mustafa amefanikiwa kufanya maonyesho Nchi tofauti za Afrika pamoja na Europa hivyo kuweza kubuni mitindo yenye ubora na hadhi ya kimataifa na kuweza kuinua soko la mitindo na mavazi nchin
Friday, March 27, 2009
Kikwete abangua Ma-DC
RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA WILAYA
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya chini kwa kuwateua wapya 15, kuwastaafisha wengine saba na kuwabadilisha vituo vya kazi 54.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) imeonyesha pia kuwa Wakuu wa Wilaya wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameteuliwa hivi karibuni kuongoza Jumuiya za Chama Tawala.
Mabadiliko haya yanatarajiwa kuongeza chachu katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake, kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa ni Bi. Mercy Silla (Arumeru, Arusha), Bw. Norman Sigalla (Hai, Kilimanjaro), Col. Issa E. Njiku (Misenyi, Kagera), Bi. Angelina Mabula (Karagwe, Kagera), Dkt. Rehema Nchimbi (Newala - Mtwara), Francis Isaac (Mbulu, Manyara), Lt. Col. Benedict K. Kitenga (Rorya, Mara) na Lt. Col. Cosmas Kayombo (Mbarali, Mbeya).
Wengine ni Bw. Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba, Mwanza); Bi. Queen Mwanshinga Mlozi (Ukerewe, Mwanza); Bi. Fatuma Mwassa (Mvomero, Morogoro); Bi. Fatma Ally (Nanyumbu, Mtwara); Bw. Juma Solomon Madaha (Tunduru, Ruvuma); Bw. Anatory Choya (Kishapu, Shinyanga) na Bw. Erasto Sima (Korogwe, Tanga).
Wakuu wa Wilaya waliostaafishwa na vituo vyao kwenye mabano ni Bw. Elias Maarugu (Misenyi, Kagera); Bw. Deusdedit Mtambalike (Muleba, Kagera); Bw. David Holela (Babati, Manyara); Bi. Hawa Ngulume (Mbarali, Mbeya); Bw. Mashimba H. Mashimba (Kyela, Mbeya); Col. Peter Madaha (Nyamagana, Mwanza) na Bw. Gilbert Dololo (Kibaha , Pwani).
Wakuu wa Wilaya ambao wamepangiwa kupewa kazi nyingine ni Bw. Patrick Tsere aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (Dar es Salaam) na Bi. Doreen Kisamo aliyekuwa Uyui (Tabora).
Bw. Martin Shigela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi (Lindi) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM wakati Bi. Husna Mwilima aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai (Kilimanjaro) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UWT.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
IJUMAA, MACHI 27, 2009.
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya chini kwa kuwateua wapya 15, kuwastaafisha wengine saba na kuwabadilisha vituo vya kazi 54.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) imeonyesha pia kuwa Wakuu wa Wilaya wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameteuliwa hivi karibuni kuongoza Jumuiya za Chama Tawala.
Mabadiliko haya yanatarajiwa kuongeza chachu katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake, kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa ni Bi. Mercy Silla (Arumeru, Arusha), Bw. Norman Sigalla (Hai, Kilimanjaro), Col. Issa E. Njiku (Misenyi, Kagera), Bi. Angelina Mabula (Karagwe, Kagera), Dkt. Rehema Nchimbi (Newala - Mtwara), Francis Isaac (Mbulu, Manyara), Lt. Col. Benedict K. Kitenga (Rorya, Mara) na Lt. Col. Cosmas Kayombo (Mbarali, Mbeya).
Wengine ni Bw. Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba, Mwanza); Bi. Queen Mwanshinga Mlozi (Ukerewe, Mwanza); Bi. Fatuma Mwassa (Mvomero, Morogoro); Bi. Fatma Ally (Nanyumbu, Mtwara); Bw. Juma Solomon Madaha (Tunduru, Ruvuma); Bw. Anatory Choya (Kishapu, Shinyanga) na Bw. Erasto Sima (Korogwe, Tanga).
Wakuu wa Wilaya waliostaafishwa na vituo vyao kwenye mabano ni Bw. Elias Maarugu (Misenyi, Kagera); Bw. Deusdedit Mtambalike (Muleba, Kagera); Bw. David Holela (Babati, Manyara); Bi. Hawa Ngulume (Mbarali, Mbeya); Bw. Mashimba H. Mashimba (Kyela, Mbeya); Col. Peter Madaha (Nyamagana, Mwanza) na Bw. Gilbert Dololo (Kibaha , Pwani).
Wakuu wa Wilaya ambao wamepangiwa kupewa kazi nyingine ni Bw. Patrick Tsere aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (Dar es Salaam) na Bi. Doreen Kisamo aliyekuwa Uyui (Tabora).
Bw. Martin Shigela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi (Lindi) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM wakati Bi. Husna Mwilima aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai (Kilimanjaro) aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UWT.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
IJUMAA, MACHI 27, 2009.
Marekani Yamtambua Anna Kilango Mwanamke Jasiri wa Kitanzania
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Larry André jana alimkabidhi cheti Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro, Mheshimiwa Anne Kilango Malecela, ambaye amechaguliwa na Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam kama Mwanamke Jasiri wa Kitanzania kwa Mwaka 2009.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Ubalozi wa Marekani, tuzo hiyo ya mwaka ilianzishwa kwa lengo la kutambua na kuthamini mchango wa mwanamke aliyeonyesha ujasiri wa kiwango cha juu na uongozi mzuri.
Aidha, Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulimteua Bi. Malecela kuwa mmojawapo kati ya washiriki waliowania Tuzo ya Kimataifa ya Mwanamke Jasiri ya Mwaka 2009, kutokana na ujasiri aliounyesha katika kukosoa na kuupa changamoto uongozi wa chama chake ili uweze kushughulikia kikamilifu suala la rushwa.
Kwa kufanya hivyo alivunja utamaduni wa kisiasa uliokuwa umejengeka bila kujali vitisho kwa usalama wake binafsi. Bila kuchoka wala kutetereka, Bi Malecela alishikilia azma yake ya kupiga vita rushwa na kuuliza maswali mazito yaliyoibua mijadala iliyochangia sana katika jitihada za kuongeza uwazi na utawala bora ndani ya chama tawala. Kwa taarifa zaidi kuhusu suala hili hebu soma hapa
Thursday, March 26, 2009
mgawo wa umeme huooooo
HAKIKA hawa jamaa wanataka kutuchezea kupita kiasi eti wameanza mchezo wa kukatakata umeme na hili shirika letu la Umeme Tanzania (Tanesco) wanadai kutakuwa na mgawo wa dharura wa umeme kwa jiji la Dar es Salaam kwa saa nane (8) zenye mahitaji makubwa ya umeme kila siku, kutokana na kile walichosema ni kukosa huduma ya mitambo miwili ya kuzalisha umeme ya kampuni ya Songas. hali hii inajitokeza katikati ya mjadala wa ununuzi wa mitambo ya Dowans na huku ikiwapo kauli ya Tanesco "tukiingia gizani tusilaumiwe" Ukitaka mambo makubwa zaidi kuhusu hii hebubonya hapa na hapa
Mzee malechela awaka
Mwanasiasa mkongwe, John Malecela, ametaka malumbano ya kisiasa yanayoendelea sasa kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakome mara moja na hayana msingi katika maendeleo ya nchi.
Malecela (75), ambaye ni Mbunge wa Mtera (CCM) pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, aliyasema hayo Dar es Salaam jana.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Sea View, Malecela alisema si vyema wala busara kuendesha malumbano kupitia vyombo vya habari ilhali kuna mamlaka zinazohusika.
“Kama mwanasiasa wa kawaida na Mtanzania, ningependa kusema kuwa malumbano haya katika vyombo vya habari, ningeomba yakome, maana hayawasaidii Watanzania,” alisema Malecela.
Aliwataka wahusika katika malumbano hayo ambayo hata hivyo hakuwataja kwa majina, watumie vyombo husika kuwasilisha hoja zao.
Alisema ni vyema kila jambo likapelekwa katika chombo husika, ambavyo ni vyama, Bunge na serikali ambako yatashughulikiwa ipasavyo na si kuwachanganya wananchi.
Malecela alisema malumbano haya huchangiwa na vyeo, fedha na mambo mbalimbali waliyonayo wanaolumbana.
Aidha, alivitaka vyombo vya habari nchini kuendelea kuelimisha jamii na kufichua maovu na si kujiingiza katika malumbano na kushabikia malumbano hayo yasiyo jenga.
“Vyombo vya habari vifanye kazi zake na visikubali kutumiwa na watu wachache na kuwaharibia hadhi yenu kitaaluma, na itafika mahali watu watadhani kuwa nia ya vyombo vya habari ni kutukanana na kuendesha mijadala isiyo na manufaa,” aliongeza.
Pia alimtaka waziri mwenye dhamana na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, achuje utitiri wa magazeti yaliyopo kwa sasa nchini ambao ni wa juu kuliko nchi yoyote barani Afrika.
Akizungumzia hoja za kumeguka kwa CCM, Malecela alisema hiyo ni ndoto na wanaotumia nukuu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ya kuwa “Mimi nang’atuka lakini ninaendelea kuamini bila CCM madhubuti nchi itayumba,” kuwa si sahihi.
Alisema iwapo kuna mwana CCM anataka kumeguka, afanye hivyo na hawatayumba kamwe na kufafanua kwa Kiingereza “we won’t miss them (hatutawajutia)” wanaotaka wajimege sasa, CCM bado ina nguvu.
Akitoa mfano wa watu waliojimega tangu kuundwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, alisema viongozi wa upinzani wote wametoka CCM lakini hakuna kilichoiharibu CCM isipokuwa imezidi kusonga mbele.
Monday, March 23, 2009
Hoteli za kitalii Paradise na Oceanic bay zateketea kwa moto
HOTELI za Paradise Holiday Resort na Oceanic Bay Hotel zenye hadhi ya nyota tatu jana ziliteketea kwa moto na kusababisha hasara ya mali ya zaidi ya shilingi bilioni 20 huku kukiwa hakuna taarifa ya watu waliojeruhiwa katika tukio hilo.
Watu walioshuhudia tukio hilo walisema chanzo cha moto huo ulioanza kuwaka saa 4.38 asubuhi, ni hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye jiko la hoteli ya Paradise na kusababisha cheche za moto zilizoruka na kukamata paa la jiko hilo kisha kusambaa kwenye maeneo yote ya hoteli hiyo na baadaye moto huo kuhamia kwenye hoteli jirani ya Oceanic Bay.
Mashuhuda hao ambao wengi wao ni wafanyakazi wa hoteli hizo mbili walisema jitihada za awali za kuudhibiti moto zilishindikana kutokana moto huo kusambaaa kwa kasi kubwa kulikochangiwa na upepo mkali wa bahari ya hindi ambapo hoteli hizo zote zimejengwa pembezoni mwa fukwe hizo huku zikiezekwa kwa paa la makuti.
Sunday, March 22, 2009
Juma Nature atoka kivyake
MSANII Juma Nature ambaye jana usiku alikuwa akizindua albamu yake ya ‘Tugawane Umasikini’ na Sauti na vyombo ya Ferouz Shaban alijaza umati mkubwa wa watu kiasi cha wengine kukosa pa kusimama. Kiujumla watu walikuwa kibao lakini kitu kimoja noma ilikuwa kwamba uzinduzi huo ulitawaliwa na harufu ya bangi katika ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya vijana kuamua kugawana bangi katika uzinduzi huo uliofanyika Jumamosi usiku.
Usiku huo ulio hudhuriwa na waheshimiwa wabunge kutoka jimbo la Temeke, Abass Mtevu na Mbunge viti Maalumu, Al-Shymaa Kwegyir ambaye aliposimama jukwaani kusalimia alishangiliwa na vijana waliyojaa ukumbimni baada ya kuwataka kupiga vita mataumizi ya viungo vya watu wenye ualemavu wa ngozo kwa imani ya kujiongezea utajiri.
Usiku huo ulitawaliwa zaidi na vijana wa umri kati ya mika 15 hadi 30 hivi kwani hukukuwa na watu wa umri mkubwa ukiacha waheshiwa ambao walikuwa wamekaa na mwanamasumbwi maarufua Mbwana Matumla aliyeambatana na mkwe kwenye meza maalumu.
Kwembe kumenuka
MDAU kutoka Kwembe ametuambia kwamba wakazi wa Kwembe Kati, Dar es Salaam wamewazuia Maofisa Ardhi kupima viwanja katika eneo lao baada ya polisi zaidi ya 20 kutawanywa katika eneo lao ili wasimamie upimaji huo badala ya kutumia kamati ya wananchi kama walivyokubaliana.
Awali wakazi hao waliwazuia watendaji hao kupima viwanja hivyo vilivyo katika mradi wa viwanja 600 juzi kwa kile walichodai kutumia polisi kulazimisha upimaji badala ya kuishirikisha kamati ya wakazi kama ilivyokubaliwa katika kikao cha pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya, Fabian Massawe, kamati na maofisa ardhi hao hivi karibuni.
Pia wakazi hao takriban 300 waliyo katika mradi huo kupitia kamati yao ya watu 10 walikubaliana na uongozi wa wilaya kupitia upya mapendekezo ambayo yanahusu fidia kwa wale ambao miundombinu kama barabara, zinapita katika maeneo yao na wenye hati tayari baada ya kuonekana wanapata viwanja vidogo kuliko makubaliano.
“Tulipeleka mapendekezo kumi ambayo yalipaswa kutolewa majibu kabla maofisa hawa hawajaja kuendelea kupima, tulitaka ufafanuzi kuhusu ramani inayotumika na namna ambavyo mipaka ya mawe inawekwa juu ya mipaka mingine, tulitaka hayo yarekebishwe lakini tunashangaa wanakuja na polisi,” alisema Jackton Manyerere mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.
“Tunampataka Kanuti (jina la kwanza ni Dioscory Kanuti-Ofisa Mipango Ardhi) atufafanulie ramani ipi inatumika maana tangu mwanzo tupo nae katika vikao na Mkuu wa Wilaya, kwa nini anatuchanganya hivi,” alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hilda Mushi ambaye ramani ya awali ilionyesha barabara inapita katikati ya nyumba yake.
Hata hivyo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Upimaji Milki Mijini, Saimon Katambi baada ya kuangalia ramani iliyokuwa inatumika, aligundua kuwa haikuwa ramani inayopaswa kutumika na ndipo alipotoa ramani halali ambapo Ndaki alipoagiza upimaji uendelee kwa ramani sahihi.
Sakata hilo lililodumu zaidi ya saa tisa, liliishia kwa wakazi hao kuwataka maofisa ardhi kukaa pamoja na kamati, Mkuu wa Wilaya na Waziri mwenye dhamana, John Chiligati, kupitia mapendekezo ya wananchi ili upiamji uendelee.
Friday, March 20, 2009
Jamaa chuo kikuu wa nchi jirani wametimuliwa
Kumbe upepo huu wa migomo hauko hapa kwetu tu hebu cheki vijana wa jirani zetu wanaendekeza libeneke mambo mbele kwa mbele si mchezo aluta continua!!! mambo yalikuwa kama hivi hebu soma hapa chini.
Kenyatta University main campus has been closed indefinitely after students there went on the rampage and stoned motorists along the busy Thika-Nairobi highway.
The students were protesting at the university’s decision to bar colleagues from registering for exams.
A circular issued by the university has ordered the students to leave the compound by the close of the day.
The students had blocked the highway for the better part of the morning to protest an ultimatum by the management to register for exams.
They told journalists that the management had given them until last Friday to pay up all their school fees and balances before they could be registered.
"But they have refused to head our pleas to be given more time to look for the money so that we can clear the balances and register for exams. The majority of students have been locked out from doing the exams," a student.
The students engaged police in running battles and stoned motorists on Thika Road. Police used teargas to chase the students who back with stones.
Nairobi head of police operations Wilfred Mbithi said police would ensure the students comply with the university order to vacate their hostels. By Cyrus Ombati and Jama Ally.
Thursday, March 19, 2009
Libeneke Miss Tanzania laanza
Vodacom Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim toka Kanda ya Ziwa-Mwanza, ambaye kazi ya kumtafuta mrishi wake imeanza kutimua vumbi akiwa katika pozi.
Meneja wa udhamini na Mawasiliano wa Vodacom George Rwehumbiza (kushoto) na Mkurugenzi wa Miss tanzania hashim Lundenga wakisaini mkataba wa udhamini kwa miaka miwili.
Rais Kikwete arejea nchini
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amerejea nyumbani leo, Alhamisi, Machi 19, 2009, akitokea London, Uingereza, ambako mwanzoni mwa wiki hii alihudhuria mkutano maalum wa maandalizi ya Mkutano wa Nchi za G-20, kuzungumzia matatizo makubwa yanayoukabili uchumi wa dunia.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Es salaam, Rais Kikwete amelakiwa na viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Rais Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi wanane wa Bara la Afrika walioalikwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown kuwakilisha msimamo wa Afrika kama nchi za Afrika zinavyoutaka uelezwe kwenye Mkutano wa G-20, uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi ujao hapo hapo London.
Viongozi wengine wa Afrika waliohudhuria mkutano huo wa maandalizi uliofanyika Jumatatu, Machi 16, 2009, kwenye Jumba la Lancaster House chini ya uenyekiti wa Gordon Brown ni pamoja na Rais Khama Ian Khama wa Botswana, na Rais Ellen Johnson Sirleaf.
Wengine ni Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Trevor Manuel, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Jean Ping, na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Donald Kaberuka.
Viongozi hao kwa pamoja walimweleza Gordon Brown msimamo wa Afrika ambao wanataka uwasilishwe katika Mkutano huo wa G-20 ikiwa ni pamoja na:
Wednesday, March 18, 2009
Mambo ya maisha plus
Mdau Pius katubandikia taarifa muhimu za vijana wetu wa Maisha Plus akisema kuwa Washiriki wawili waliokuwa wakiwakilisha kanda ya kati, Efrancia Mangii (kulia) na Peter Putir (Shoto) wameliaga shindano la Maisha Plus hilo huku Maulid Wadi akirejea baada ya kupata kura nyingi.
Washiriki hao wamefungua dimba la kuaga katika shindano hilo lililoanza wiki mbili zilizopita. Shindano hilo linabakiwa na mshiriki mmoja anayewakilisha kanda hiyo, Juma Madaraka.
Wakati huohuo Putir ameapta shavu la kutangaza katika kituo cha redio cha TBC Fm mara baada ya utolewa katia shindano hilo.
Mkurugenzi wa TBC, Tido Mhando aliitangaza ofa hiyo wa Putir baada ya uvutiwa na sauti nzuri ya mshiriki huyo.
Washiriki hao wamefungua dimba la kuaga katika shindano hilo lililoanza wiki mbili zilizopita. Shindano hilo linabakiwa na mshiriki mmoja anayewakilisha kanda hiyo, Juma Madaraka.
Wakati huohuo Putir ameapta shavu la kutangaza katika kituo cha redio cha TBC Fm mara baada ya utolewa katia shindano hilo.
Mkurugenzi wa TBC, Tido Mhando aliitangaza ofa hiyo wa Putir baada ya uvutiwa na sauti nzuri ya mshiriki huyo.
Ajali nyingine yaua 10 Mbeya
Taarifa zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kuwa lori la mizigo likiwa linatokea eneo la Nzovwe kuelekea mjini limegonga magari sita na kusababisha vifo zaidi ya 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 10.
Watu waliofika katika eneo hilo wametueleza kuwa kuwa lori hilo liligonga magari hayo baada ya kukosa breki na kuserereka umbali mrefu kabla ya kuyaparamia magari mengine matano madogo ya abiria. Habari zaidi soma Mwananchi.
Malya afungwa miaka mitatu
Deus Mallya aliyedaiwa kuwa dereva wa Marehemu Chacha wangwe, Mbunge wa Tarime aliyekufa katika ajali njiani akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam, amehukumiwa mvua tatu jela (miaka mitatu) na Hakimu Mkazi wa Dodoma.
Mallya amekutwa na hatia ya kuendesha gari bila leseni na kusababisha kifo cha Mbunge huyo.
Wakili aliyekuwa anamtetea, Godfrey Wasonga alijikuta akitokwa na machozi baada ya mahakama kutamka kuwa imemtia hatiani kwenye mahakama hiyo ambayo ilifurika watu wengi waliofika kusikiliza hukumu hiyo.
Hakimu Mkazi, Thomas Simba alisema kuwa mahakama imeridhika pasipo na shaka kuwa kijana huyo ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo na kwamba kifo cha marehemu kilitokana na mwendo kasi.
Baada ya hakimu kusoma maelezo hayo wakili wa mshitakiwa Godfrey Wasonga alianza kulia hali iliyoonyesha kuwa alikwisha ona mwelekeo wa kesi hiyo unamuendea vibaya mteja wake.
Hakimu alisema kuwa kutokana na sheria ya makosa ya usalama barabarani iliyofanyiwa marekebisho na bunge mwaka 2002 namba 63 kifungu cha pili kifungu kidogo (a) inasema kuwa kutokana na makosa yanayofanana na makosa ya mtuhumiwa, adhabu yake inaanzia miaka mitatu na kuendelea.
Hakimu huyo alisema kuwa kutokana na utetezi wa mshitakiwa ameamua kumfunga miaka mitatu kwa kosa la kuendesha gari mwendo kasi na kusababisha ajali.
Aliendelea kusema kuwa kwa kosa la kuendesha gari bila ya kuwa na leseni mahakama inamhukumu kwenda jela mwaka mmoja lakini akasemakuwa adhabu hizo zinakwenda pamoja, hivyo atatumikia kifungo cha miakamitatu gerezani.
Alisema kuwa kifo cha Wangwe kilisababishwa na mlango wa kushotoambao ulimbana na kufafanua kuwa ushahidi ulithibitisha kuwa marehemu hakuwa analiendesha gari hilo.
Tuesday, March 17, 2009
Papa Benedicto aanza ziara ya Afrika
Papa Benedict XVI akipanda ngazi kuelekea katika ndege yake maalum kwenye uwanja wa ndege wa Fiumincino, Roma kwa ajili ya kuanza safari yake katika ziara ya siku sita barani Afrika jana asubuhi. Atatembelea nchi za Cameroon na Angola.
Reuters
Reuters
VATICAN, Italy
KIONGOZI mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Benedict XVI ameanza ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu alipokabidhiwa wadhifa huo, huku akieleza kuwa suala la usambazaji wa kondomu si jibu sahihi dhidi ya Ukimwi.
Akiwa njiani kuelekea nchini Cameroon, sehemu ya kwanza katika ziara yake hiyo ya siku sita kwa Afrika, Papa Benedict alisema kuwa kanisa lake litaendelea kusimama mstari wa mbele kupambana dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa Afrika kwa kutumia misingi ya wazi ya kitabu kitakatifu cha Biblia.
Ziara hiyo ya Papa ni ya kwanza kwa Afrika tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo ya juu kwa kanisa Katoliki duniani miaka minne iliyopita, huku akieleza kuwa “hakuna uwezekana wa kutokomeza maambukizi ya ukimwi kwa kuhamasisha matumizi ya kondom, zaidi kwa kufanya hivyo ni kuongeza ukubwa wa tatizo,” alisema wakati akiwa kwenye ndege yake mara baada ya kuanza safari kuelekea Cameroon.
Kama hakutatokea mabadiliko katika ziara yake hiyo, Papa atatumia siku sita za ziara yake katika nchi za Cameroon na Angola, huku taarifa zikieleza kuwa hali katika mji mkuu wa Cameroon, Younde, ulio kituo cha kwanza cha Papa uko katika tahadhari ya hali ya juu.
KIONGOZI mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Benedict XVI ameanza ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu alipokabidhiwa wadhifa huo, huku akieleza kuwa suala la usambazaji wa kondomu si jibu sahihi dhidi ya Ukimwi.
Akiwa njiani kuelekea nchini Cameroon, sehemu ya kwanza katika ziara yake hiyo ya siku sita kwa Afrika, Papa Benedict alisema kuwa kanisa lake litaendelea kusimama mstari wa mbele kupambana dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa Afrika kwa kutumia misingi ya wazi ya kitabu kitakatifu cha Biblia.
Ziara hiyo ya Papa ni ya kwanza kwa Afrika tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo ya juu kwa kanisa Katoliki duniani miaka minne iliyopita, huku akieleza kuwa “hakuna uwezekana wa kutokomeza maambukizi ya ukimwi kwa kuhamasisha matumizi ya kondom, zaidi kwa kufanya hivyo ni kuongeza ukubwa wa tatizo,” alisema wakati akiwa kwenye ndege yake mara baada ya kuanza safari kuelekea Cameroon.
Kama hakutatokea mabadiliko katika ziara yake hiyo, Papa atatumia siku sita za ziara yake katika nchi za Cameroon na Angola, huku taarifa zikieleza kuwa hali katika mji mkuu wa Cameroon, Younde, ulio kituo cha kwanza cha Papa uko katika tahadhari ya hali ya juu.
Rais wa Ravalomanana ajiuzulu
ANTANANARIVO, Madagascar
RAIS wa Madagascar Mark Ravalomanana amejiuzulu na kukabidhi nchi kwa jeshi la nchi hiyo baada ya sekeseke lililodumu ndani ya taifa hilo kwa muda sasa na baada ya kiongozi wa upinzani wa taifa hilo, Andry Rajoelina kuanzisha vuguvugu na kuungwa mkono na jeshi la taifa hilo na sasa ameingia katika ofisi maalum za rais wa nchi hiyo, siku moja baada ya kikosi cha skari wanaomuunga mkono kuziteka na kuzishikilia ofisi hizo.
Muda mfupi baada ya kuingia katika ofisi hizo, Rajoelina aliwaeleza wafuasi wake kuwa tayari mawaziri nane wa rais halali wa nchi hiyo, Mark Ravalomanana wamewasi.lisha kwake barua zao za kujiuzulu, baada ya kuona kwua mamlaka ya Ravalomanana imepoteza nguvu.
Rajoelina ameiongia katika ofisi hizo za rais katika majengo hatyo yaliyoshikilwia na askari wanaomtii, huki umbali wa kilomita 12 kutoka mji mkuu Antananarivo, Rais Ravalomanana amejifungia katika kasri jingine la rais huko Iavoloha, akizungukwa na kikosi chake maalum na baadhi ya wafuasi wake.
Ravalomanana tayari amepuuza woto na ushauri kutoka wka watu wake wa karibu kumtaka akimbilie uhamishoni na kupinga kung'atuka, huki akieleza kuwa atatetea haki yake hadi kufa, huku walinzi na wafuasi wake wakiwa wamezifunga njia zote zinazoelekea eneo hilo.
"Rais ameamua kusalia Madagascar, ameshawaambia walinzi wake waliomshauri akimbilie uhamishoni kuwa tatetea haki hata ikibidi mpaka kufa. Hii inaelekea kuwa njama ya mapinduzi ya kijeshi,” msemaji wa ofisi ya rais Ravalomanaan alieleza.
Monday, March 16, 2009
Juma Nature kuzindua
Sunday, March 15, 2009
Mzee Shaaban Mloo afariki dunia
The Civic United Front (CUF – Chama cha Wananchi) kinasikitika kuwaarifuni kwamba, leo asubuhi mwasisi wa chama hiki, Shaaban Khamis Mloo, amefariki dunia, nyumbani kwake, mjini Zanzibar. Mazishi yake yalifanyika jana saa 10.00 alasiri huko huko Zanzibar.
Marehemu Mzee Mloo alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa CUF kwa miaka nane, kutoka 1992 hadi 2000 alipochukua nafasi ya umakamo mwenyekiti hadi alistaafu mwaka 2004. Yeye ndiye miongoni mwa waasisi wa Chama hiki, kwa kuanzia na vuguvugu la KAMAHURU. Ni yeye ndiye aliyeongoza mazungumzo ya kwanza na aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CCW), James Mapalala, na hatimaye kuungana na kuzaliwa kwa CUF tuliyonayo sasa.
Kwa hivyo, CUF inamtambua Mzee Mloo sio tu kama kiongozi mstaafu wa Chama, bali zaidi kama mwasisi, mwanzilishi na mwanachama imara na shupavu katika siku zote za uhai wake. Atakumbukwa daima ndani na nje ya CUF kama mjuzi wa siasa za Zanzibar na za Tanzania kwa ujumla, mchapakazi na mtu aliyekuwa na ujasiri wa kupigiwa mfano.
Hata baada ya kustaafu umakamo mwenyekiti, Mzee Mloo aliendelea kuwa sehemu muhimu ya CUF kwa kujitolea katika mashauri mbali mbali. Kila alipokuwa na uwezo, hakuacha kuhudhuria mikutano ya hadhara au vikao vyovyote ambavyo alialikwa.
Kikao cha mwisho kuhudhuria ni Mkutano Mkuu wa Nne wa chama chetu uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, kuanzia 23 hadi 27 Februari, mwaka huu. Kwa hivyo, hadi siku za mwisho mwisho wa uhai wake, Mzee Mloo alisimama imara kuijenga na kuihuisha CUF.
Friday, March 13, 2009
Mkasa wa Raisi mstaafu Mwinyi kupigwa kibao
Haka kajamaa kalikosa akili kabisa na adabu mbele ya wakubwa, hata kama imani imekaingia vipi, lakini kalichokifanya ni kichaaa na utofu wa adabu wa kiwangu kikubwa, taarifa zilizonifikia hivi sasa ni kwamba haka kajamaa kalikomzaba mzee mwinyi kibao kamefungwa jela mwaka mmoja kama fundisho kwake na wengine wenye adabu ndogo kama kenyewe. CLIP HII IMETOLEWA KWA HISANI YA MDAU TANGI BOVU.
Ziara ya waziri Mkuu
Subscribe to:
Posts (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...