Tuesday, November 15, 2016

WAZIRI WA MALIASILI, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MISITU KUJADILI UHAMASISHAJI NA UENDELEZAJI SEKTA HIYO KATI YA TANZANIA NA FINLAND

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kikanda wa Wadau wa Sekta ya Misitu wa nchi ya Finland na Tanzania uliofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam. Lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kuhamasisha uwekezaji na kukuza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika uendelezaji wa misitu nchini. Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, Taasisi ya Uongozi - UONGOZI Institute na Shirika la Maendeleo ya Kifenda la Finland - FINFUND. 
Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Serikali ya Finland, Kai Mykanen akizungumza katika Mkutano huo ambapo ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya  Finland na Tanzania katika kuendeleza Misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho ikiwa ni pamoja na kukuza teknolojia ya uhifadhi wa mazingira ya kupunguza hewa ukaa. 
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Eng. Angelina Madete na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.
Baadhi ya wajumbe katika mkutano huo wakifualia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Finland ikiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo, Kai Mykanen (wa pili kushoto) muda mfupi kabla ya ufunguzi wa mkutano huo. Wengine kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mehenge, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali, Gaudence Milanzi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano huo. Alieleza kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa misitu unaotokana na uvunaji wa mkaa na ukataji wa magogo, uvunaji wa miti usio endelevu jambo lililoisukuma Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Finland na wananchi kwa ujumla kwa ajili kuendeleza misitu kwa kupanda miti mingi zaidi iweze kukidhi mahitaji yaliyopo. Aliongeza kuwa ni marufuku kusafirisha magogo na kwamba Serikali ya awamu ya tano imelenga kukuza viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani kwenye mazao ya misitu na kuyauza kama bidhaa. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanzi na kulia kwake ni Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja.(Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili naUtalii)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...