Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka kwa Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Athumani Salum (kulia) jijjini Dar es Salaam. Picha hiyo imechorwa kwa ustadi na kikundi cha Angavu Youth Group.
Muonekano wa picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli iliyoichora kwa ustadi na kikundi cha Angavu Youth Group ambapo imekabidhiwa jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye kwa niaba ya Mheshimiwa Rais.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya makabidhiano ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli iliyochorwa na kikundi cha Angavu Youth Group jijini Dar es Salaam. Picha hiyo imekabidhiwa kwa Waziri huyo kwa niaba ya Mhe. Rais. kushoto ni Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Bw. Athumani Salum na kulia ni Katibu wake Bi. Oliver Charles.Picha na Anitha Jonas – MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikisomwa na Katibu wa Angavu Youth Group Bi.Oliver Charles (katikati) wakati wa makabidhiano ya picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment