Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ameeleza kuwa mswada mwingine utakaojadiliwa ni mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali pamoja na wabunge kutoa ushauri kwa serikali kuhusu vyanzo vya mapato na vipaumbele vya bajeti ya mwaka 2017/18 ambayo itajadiliwa siku tatu mfululizo.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai.
Mh. Ndugai amesema katika mkutano wa tano wabunge pia wataishauri serikali kuhusiana na mkataba wa makubaliano wa ushirikiano kiuchumi na ulaya.
Miongoni mwa yaliyojiri
- Swali kutoka kwa mbunge Juma Nkamia na swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge Freeman Mbowe kuhusu pesa zilizoahidiwa na serikali kuzipa milioni 50 kila kijiji.
- Waziri kasema fedha hizo zipo na wanafanya utaratibu kuweza kufika na kutumiwa kulingana na makusudio.
- Ugawaji TZS mil 50/- kila kijiji zinasubiri kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri ambalo litajadili mfumo utakaotumika.
- Waziri Mhagama: Katika bajeti ya 2016/17, serikali imetenga kiasi cha TZS bilioni 59.5 kwa ajili ya kugawa fedha kwa kila kijiji.
- Naibu Waziri wa Afya Kigwangala: Hakuna shehena ya madawa iliyozuiliwa ,dawa zipo na zinapatikana kwa asilimia 100% kote nchini.
Swali: Mpwapwa vijiji vingi vina tatizo la maji, serikali ina mpango gani kuchimba visima?
Jibu: Serikali imetenga bilioni 1.58 kujenga visima Mpwapwa na kukarabati miundombinu iliyopo
Jibu: Serikali imetenga bilioni 1.58 kujenga visima Mpwapwa na kukarabati miundombinu iliyopo
Swali: Serikali ina mpango gani waliosababisha watumishi hewa
Majibu(Kairuki): Serikali imechukua hatua kwa watumishi 1663 waliobainika kusababisha watumishi hewa kwa vyombo vya usalama na mamlaka zao za kinidhamu.
Nyongeza (Maida): Nawapongeza serikali wanavyojitahidi, katika uhakiki ni hasara kiasi gani serikali imepata mpaka tarehe tajwa? Serikali inaweza kuwapa adhabu ya kurudisha fedha zilizopotea?
Majibu (Kairuki): Hadi sasa watumishi hewa 19,629 wameondolewa ambao kama wangebaki wangeisababishia serikali hasara ya bilioni 19 kila mwezi. Kwa ambao mashauri yao yapo mahakamani wametakiwa kulipa faini au kurudisha fedha na watakaoshindwa kufungwa jela.
Swali la Nyongeza: Serikali inapaswa ijazie nafasi kwa watumishi wapya ikiwemo wanafunzi wanaomaliza lakini hadi leo mikopo haijatoka.
Majibu (Stella Manyanya): Kama inavyosisitizwa, pesa za mikopo Tshs bilioni 80 zimeshatolewa na kilichotuchelesha ni uhakiki, fedha inayotolewa ni kwa wale wenye uhitaji kupita wenzao. Wale wote wanaostahili kupata mikopo watapata na ndani ya wiki hii tutakuwa tumefikia mahali mazuri zaidi. Serikali inashughulikia mambo mengi katika sekta ya elimu na siyo mikopo pekee, kwa hiyo pesa nyingine zinatumika kwenye mambo mengine kama vile ujenzi wa mabweni, maabara na miundombinu mingine.
Mwenyekiti wa Bunge: Pamoja na majibu mazuri tunaomba tamko la serikali kuhusu mikopo ya wanafunzi
Swali (Waitara): Serikali ina mpango gani wa dharura wa kupunguza gharama za upimaji ardhi ili wananchi wengi
Jibu: Upimaji hufanywa na wapimaji wa serikali na binafsi waliopewa leseni. Laki tatu kwa hecta moja ya shamba au kiwanja kimoja ambapo kabla ilikuwa laki 8 kwa hekta. Vifaa vya upimaji ni gharama kubwa sana hivyo wapimaji wengi kukodi kwa gharama kubwa, kukabiliana na ongezeko, serikali kusogeza huduma kwenda kwenye kanda.
Nyongeza (Waitara): Nilimuita mpimaji chini ya ekari mbili ikawa Milioni 5, naomba maelekezo. Migogoro mingi ni kwa sababu sehemu kubwa haijapimwa, mpango wa kusogeza huduma kuna bajeti imetengwa?
Jibu (Naibu Waziri): Laki tatu kwa hekta ndio gharama sahihi baada ya bunge hili kuzipunguza, kama manispaa ina tozo tofauti inategemea halmashauri hiyo wamekubaliana nini!
Bashe: Kata za Nzega mjini zilikuwa zipelekewe umeme kwa fedha za MCC na miradi imefutwa, waziri anawaambia nini?
Jibu: Miradi yote iliyokuwa chini ya MCC itapelekwa na pesa za REA ikiwemo kata za jimbo la mheshimiwa Bashe.
No comments:
Post a Comment