Tuesday, November 08, 2016

MFUMUKO WA BEI WA MWEZI OKTOBA 2016WALINGANA NA MFUMUKO WA BEI SEPTEMBER 2016

Na Antony John blog jamii.


Ofisi ya Taifa ya takwimu imeeleza Kuwa mfumoko wa bei wa Taifa wa mwezi Octoba 2016 umebadilika Kwa asilimia 4.5 Kama ulivyokuwa September 2016.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Mtakwimu kutoka ofisi ya Taifa ya takwimu Bi,Ruth Minja amesema Kuwa kubaki Kwa asilimia 4.5 kunamaanisha kasi ya upandaji bei Kwa bidhaa na huduma Kwa mwezi Octoba umekuwa sawa Kwa kasi ya upandaji wa Mwaka ulioishia mwezi September 2016.

   Mtakwimu huyo amefafanua Kuwa mfumuko wa bei Kwa mwezi Octoba 2016 imechangiwa na kuongezeka Kwa kasi ya bei ya baadhi ya bidhaa Za vyakula na zisizo Za vyakula kipindi kilicho ishia mwezi Oktoba 2016  zikilinganishwa na bei Za mwezi Octoba 2015 ambapo Mwenendo wa bidhaa Za vyakula zilizoonesha kuongezeka ni pamoja na mahindi Kwa asilimia 18.3, unga wa ngano Kwa asilimia 4.8, samaki wa bichi Kwa 5.07, ndizi za kupika Kwa asilimia 5.2, Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula  kama Mkaa umeongezeka Kwa asilimia 15.4 na vyakula kwenye migahawa vimeongezeka Kwa asilimia 17.3.

    Minja ameongeza Kuwa fahirisi Za bei zimeongeka Hadi asilimia 103.17 mwezi Oktoba 2016 kutoka 103.05 mwezi September 2016 kuongezeka Kwa fahilisi Za bei kumechangiwa na kuongezeka Kwa bei Za baadhi ya bidhaa Za vyakula na bidhaa zisizo Za vyakula bidha Za vyakula zilizo changia kuongezeka Ni samaki wa bichi Kwa asilimia 9.8. Mihogo Kwa asilimia 9.7, mahindi Kwa asilimia 4.7 Katanga Kwa asilimia 3.7, maharage Kwa asilimia 3.8. Huku Kwa bidhaa zisizo Za vyakula fahilisi zilizo ongezeka Ni gharama ya kodi ya pango Kwaajili ya makazi Kwa asilimia 2.9 na Mkaa Kwa asilimia 1.1,

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...