Tuesday, November 15, 2016

MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN ASAFINI NA NDEGE YA AIR TANZANIA KUELEKEA JIJINI MWANZA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa tiketi ya kusafiria ya Shirika la Ndege la Air Tanzania, kutoka kwa Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Professa Makame Mbarawa, kabla ya kusafiri na Ndege hiyo kuelekea Jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi, Novemba 14, 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na marubani na wahudumu wa ndege mpya aina ya Bombardeir Q 400 baada ya kukabidhiwa ticket ya kusafiria na Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Professa Makame Mbarawa kulia Novemba 14, 2016 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ambapo Makamu wa Rais alisafiri na ndege hiyo kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na vyombo vya habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipungia wakati akiindia ndani ya Ndege ya Air Tanzania aina ya Bombardeir Q 400.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya Abiria waliokuwemo ndani ya Ndege hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Mwanza na kwa mara ya kwanza umetumia usafiri ya ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya bombardier Q400 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ambapo ndege hiyo pia ilibeba abiria wa kawaida katika safari hiyo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kusafiri na baada ya kuwasili mkoani Mwanza amewahimiza wananchi kutumia usafiri wa ndege za ATCL kwa sababu ni wa bei nafuu na usafiri wake ni wa uhakika.

Amesema kwa kutumia ndege ya ACTL imemsaidia kupunguza gharama kubwa ya usafiri kwa kutumia ndege za binafsi za kukodi kwa ajili ya safari za kikazi za ndani ya nchi.

“Ni ndege zetu ni fahari yetu zipo Tanzania ni lazima sisi Watanzania tuzitumie ipasavyo kusafiria ndio maana na mimi leo nimeamua kutumia usafiri wa ATCL kwa sababu ni mzuri na wa uhakika”

Makamu wa Rais amesema amefurahi kusafiri kwa mara ya kwanza na ndege hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na amehimiza viongozi na wananchi kwa ujumla kutumia usafiri wa ndege za ATCL ili kulipa nguvu shirika hilo katika ufanyaji wake wa kazi kwa viwango bora zaidi.

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Mwanza, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali na wa vyama vya siasa ambao waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Akiwa mkoani Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi siku NNE mkoani humo katika  wilaya za Ukerewe,Ilemela,Nyamagana, Misungwi,Kwimba na Magu.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...