Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MWILI wa aliyekuwa Waziri Mstaafu Joseph Mungai unatarajiwa kuagwa kesho katika Viwanja vya Karimjee majira ya saa tano asubuhi na kisha kusafirishwa kuelekea Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa kwa ajili ya mazishi.
MWILI wa aliyekuwa Waziri Mstaafu Joseph Mungai unatarajiwa kuagwa kesho katika Viwanja vya Karimjee majira ya saa tano asubuhi na kisha kusafirishwa kuelekea Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa kwa ajili ya mazishi.
Mungai aliyezaliwa Oktoba 24,1943 alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi aliwahi kuwa Mbunge wa Mufindi kupitia CCM kwa kipindi cha miaka 35 na kufanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali serikalini enzi za utawala wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na pia katika awamu za pili.
Baadhi ya nyadhifa alizowahi kushika kwa nyakati tofauti ni uwaziri wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwanasiasa mkongwe Chrisant Mzindakaya amesema kuwa wataendelea kumkumbuka Mungai kwani moja ya wanasiasa waliokuwa na msimamo na aliweza kufanya mageuzi katika wizara alizokuwa anafanyia kazi hususani wizara ya Kilimo na pia hakuwa na kusubiri kesho kama kuna jambo analoweza kulifanya leo hawezi kusubiri kesho.
Mtoto wa tatu wa marehemu,William Mungai amesema kuwa baada ya utaratibu wa kuaga mwili wa marehemu pale Karimjee watasafiri kuelekea Mkoani Iringa kwa ajili ya mazishi yanayitarajiwa kufanyika Jumamosi majira ya saa nane mchana.
No comments:
Post a Comment