Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza kwenye
kikao cha majadiliano ya manunuzi ya nyumba za gharama nafuu NHC Uyui, Tabora.
Kikao hicho kimefanyika makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC PLACE
ambapo kikao kiliwashirikisha Wabunge wa Igalula Mussa Ntimizi, Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini, wilaya ya
Uyui mkoani Tabora Mheshimiwa Almasi Maige na madiwani wa Uyui na makubaliano
yamefikiwa kwa wajumbe hao kukubaliana kununua nyumba 32 huku taratibu zingine
zikiendelea nyumba zilizobakia 17 zitafuata utaratibu mwingine. Kulia kwake ni
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria cha NHC, Martin Mdoe.
Timu ya viongozi wa Wilaya ya Uyui wakifuatilia kwa karibu maelezo ya kina yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu kabla ya kufikia makubaliano yaliyofikiwa na viongozi hao.
Uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu kabla ya kufikia makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa Uyui.
Timu ya viongozi wa Wilaya ya Uyui ikiongozwa na Wabunge wa Igalula Mussa Ntimizi, Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini, wilaya ya Uyui mkoani Tabora Mheshimiwa Almasi Maige, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uyui, Said Shaban Ntahondi na madiwani wa Tabora Kaskazini nwakifuatilia kwa karibu maelezo ya kina yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu kabla ya kufikia makubaliano yaliyofikiwa na viongozi hao.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza kwenye kikao cha majadiliano ya manunuzi ya nyumba za gharama nafuu Uyui, Tabora.
No comments:
Post a Comment