Monday, November 14, 2016

Kuelekea uchumi wa viwanda na biashara; Wadau waaswa kuwekeza kwenye viwango vya kimataifa.

 Mwakilishi wa kampuni ya Bureu Veritas inayosimamia uhakiki wa viwango vya kimataifa (Certfying board)  Bw Boniface Githae (wa pili kulia) akikabidhi cheti cha ubora wa kimataifa kutoka Shirika la Viwango Duniani (ISO) yaani ISO 9001:2008 Certification kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe (wa pili kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni Mwenyekiti wa kampuni ya Amen Consulting Ltd Dk. Benjamin Sirimba (wa kwanza kushoto)ambae  kampuni yake ndio ilitoa muongozo kwa kampuni ya ZH Poppe kupata cheti hicho na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bw Hassan Atako.
Wanawake wanaweza! Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na dereva pekee wa kike kwenye kampuni hiyo.
Ikawa ni kujipongeza ni kujipongeza tu!


Familia nayo haikuwa nyuma… Hongera Babu!
Mwenyekiti wa kampuni ya Amen Consulting Ltd Dk. Benjamin Sirimba (wa kwanza kulia)ambae  kampuni yake ndio ilitoa muongozo kwa kampuni ya ZH Poppe kupata cheti hicho akitoa nasaha zake wakati wa hafla hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe akitoa nasaha zake kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa.
Timu ya Ushindi! Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwemo madereva mara baada ya kukabidhiwa cheti hicho, 

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa kampuni hiyo mara baada ya kukabidhiwa cheti hicho.
Wadau wakijipongeza!

KUELEKEA uchumi wa viwanda na biashara hapa nchini, mashirika ya umma, taasisi binafsi na makampuni mbalimbali yameombwa kuwekeza katika utoaji wa huduma zinazokidhi viwango vya kimataifa ili kwenda sambamba na matakwa ya kiushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa kampuni ya Amen Consulting Ltd Dk. Benjamin Sirimba wakati wa hafla fupi ya kukabidhi cheti cha wa  ubora kimataifa kutoka Shirika la Viwango Duniani (ISO) yaani ISO 9001:2008 Certification hicho kwa kampuni ya usafirishaji ya ZH Poppe Ltd ya jijini Dar es Salaam.

“Ustawi wa uchumi wa viwanda na biashara hapa nchini utakwenda sambamba na ongezeko la ushindani wa kibiashara pia hivyo suluhisho la msingi katika kuishi kwenye soko hilo ni kutafuta masoko nje hatua ambayo ili kufanikiwa muhusika anatakiwa akidhi  viwango vya ubora wa kimataifa na hapo ndipo unapokuja umuhimu wa kuwa na cheti hiki,’’ alibainisha.

Kwa mujibu wa Dk Sirimba ambae  kampuni yake kwa kushirikiana  na Consumer Pride Africa inatoa mwongozo na mafunzo kwa makampuni binafsi na mashirika ya umma hapa nchini ili yaweze kupata vyeti vya ubora yaani cha ISO, utolewaji wa cheti  hicho kwa kampuni ya ZH Poppe Ltd, ulifuatia kampuni hiyo kukidhi vigezo vyote vinavyohitajika baada ya kufanya vizuri na kufuzu katika mafunzo ya miezi sita yaliyotolewa kwa watendaji wa kampuni hiyo katika nyanja mbambali za kimfumo na kiutendaji.

Akizungumza mara baada ya kupokea cheti hicho, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ZH Poppe Ltd, Bw Zacharia Poppe alisema si tu kwamba kinaonyesha ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo katika usafirishaji wa mizigo ya aina mbalimbali ndani na nje ya nchi bali pia kitaongeza chachu katika kuhakikisha kwamba kampuni hiyo inafikia malengo yake ya kutoa huduma zaidi nje ya mipaka ya nchi.

“Kwa kuwa cheti  hiki kilitanguliwa na mafunzo kwa watumishi wa idara zote wakiwemo madereva wetu tafsiri yake ni kwamba tofauti itaonekana hata huko barabarani kwa maana kwamba tunatarajia ajali zitokanazo na uzembe zitapungua kama sio kwisha kabisa,’’ alisema Bw Poppe huku akiwasihi madereva wa kampuni hiyo kuzingatia mafunzo waliyoyapata katika mchakato wa kupata cheti hicho.

Akizungumzia cheti hicho Mwakilishi wa kampuni ya Bureu Veritas inayosimamia uhakiki wa viwango vya kimataifa (Certfying board)  Bw Boniface Githae alisema cheti hicho kinatolewa kwa mashirika, taasisi na makampuni baada ya kithitibishwa kuwa  yamekidhi vigezo vya kimataifa katika kutoa huduma zao, uthibitisho unaotanguliwa na mafunzo mbalimbali kwa watumishi na viongozi na mashirika husika.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...