Tuesday, November 29, 2016

WAZIRI LWENGE ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MABOMBA NCHINI

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiangalia aina ya bomba lililotumika kwenye mradi wa Ruvu Chini na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh (kulia) pamoja na Meneja Biashara, Ryan Koh.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye karakana ya kiwanda hicho.
Mafundi wakiwa kazini katika karakana ya Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh na kujionea moja ya mabomba yanayotengenezwa na kiwanda hicho.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge mwishoni mwa wiki alitembelea Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP) kilichopo Shekilango, Dar es Salaam.

Kiwanda hicho kinachotengeneza mabomba ya maji, ambayo pia yanatumika katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini, ukiwemo mradi ya maji ya Ruvu Chini, KASHWASA na Ruvuma.

“Nimeridhishwa na uwekezaji wa kiwanda hiki cha mabomba, ambacho kina uwezo wa kuzalisha mabomba yenye ubora wa kutekeleza miradi yetu ya maji nchini”.“Hii ni hatua kubwa kwa nchi yetu ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuinua uchumi wa viwanda nchini, hivyo maendeleo ya kiwanda hiki ni hatua nzuri ya kufikia lengo hilo”, alisema Waziri Lwenge.

Inj. Lwenge alisema uwezo ilionao kiwanda hiki ni chachu ya maendeleo kwa Sekta ya Maji na Umwagiliaji kwani kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikununua mabomba kutoka nje ya nchi, na hata yanayotengenezwa hapa mengi ni ya plastiki ambayo hayadumu muda mrefu ukilinganisha na ya chuma.Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP) alisema nia yao kubwa ni kutengeneza bidhaa nzuri zenye ubora wa kimataifa na kushindana katika soko la kimataifa, na kuiomba Serikali itumie bidhaa za wawekezaji wa ndani zenye ubora wa hali ya juu.

Alisisitiza bidhaa zao zinatengenezwa hapa nchini tangu hatua ya awali na wala si kuagizwa kutoka nje, zina uwezo wa kudumu mpaka miaka 50, zinatumika nje ya nchi ikiwemo Rwanda, ambapo zinatumika kwenye miradi mikubwa ya maji.Dhumuni la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea uwezo wa kiwanda hicho kwa upande wa uzalishaji na ubora wa bidhaa zao.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...