Wednesday, November 02, 2016

Asilimia 85 ya Ardhi nchini haijapimwa,Watu wengi wanaendelea kuishi katika makazi holela-Waziri Lukuvi

Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akifungua mkutano mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi linalofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia leo Novemva 2-3, 2016.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akionyeshwa moja ya vifaa vinavyotumika katika upimaji wa Ardhi mapema leo katika Mkutano mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akipewa maelezo jinsi mambo yalivyobadirika katika mfumo wa Kidigitali.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiwa amebeba moja ya kifaa kinachotumika katika upimaji.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akionyeshwa kifaa cha kisasa kinachotumika katika upimaji.
Wapimaji wa Ardhi wakiwa katika mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi.
Wapimaji wa Ardhi wakiwa katika mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akitoa cheti cha shukrani kwa makampuni yaliweza kusaidia kufanikisha mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi. Pembeni kushoto ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Bw. Justo Lyamuya.
 
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii.
 
Hayo ameyasema leo Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi wakati akifungua Mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi uliofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa wataalam wafanye kazi ya kupima ardhi ili kuweza kuondokana na makazi holela.

Amesema kuwa serikali inapoteza mapato kutokana na kuwa na sehemu kubwa ya ardhi kutopimwa.Lukuvi amesema wapimaji wa sekta binafsi wamekuwa wakifanya vizuri kuliko wale ambao wameajiliwa na serikali.

Amesema lazima kuondokana na mfumo wa hati kwenye karatasi na kuingia katika mfumo wa kieletroniki katika kusaidia wananchi kudhulumiwa ardhi kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu.

Waziri Lukuvi amesema ni marufuku kwa wapimaji ardhi walioajiliwa na serikali kuwa kampuni za upimaji wa ardhi ili kuondokana na mgongano wa kimasilahi. Amesema katika miaka 10 ijayo kuwa kila mtu kuwa hati na kiwanja au shamba kiwe kimepimwa.Lukuvi amesema katika kuondoa migogoro ya wafugaji ni kuondokana na uchungaji wa mifugo.

Amesema kufika mwishoni mwa mwaka huu wawe wamepima ardhi viwanja 400.Nae Rais IST, Martins Chodata amesema kuwa watashirikiana na serikali katika masuala ya upimaji ardhi.Amesema wapo baadhi ya wapimaji ardhi hawana maadili na kusababisha kuwepo migogoro. 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...