Friday, January 31, 2014

WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII, WATEMBELEA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII, RUNGEMBA IRINGA. RUNGEMBA

imageNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (mb.) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa,Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii leo wametembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa.  Lengo la ziara hii ni kukagua utekelezaji wa shughuli za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika utoaji wa Mafunzo ya Maendeleo ya Jamii kupitia chuo hiki. Katika ziara hii, wajumbe wa kamati walipata fursa ya kupokea taarifa ya chuo na kutembelea maeneo / miradi mbalimbali ya chuo.image_1Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii  wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe.Saidi Mtanda (Mb.) wakikagua maeneo / miradi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na kutoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, katika baadhi ya maeneo yenye kuhitaji maboresho.image_2Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Kati) pamoja na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba, (Kulia, mwenye nguo ya kahawia) Bibi Santina Mbata wakiwapitisha Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Majengo / miradi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...