Monday, January 20, 2014

MTEMVU AWANDALIA MSOSI MARAFIKI ZAKE KUTOKA CHUO KIKUU CHA BUFFALO MAREKANI

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto) na Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Buffalo cha Marekani, Tyler Choi wakati wa hafla ya chakula cha usiki alichowaandalia marafiki zake hao  jana kwenye Hoteli ya Sea Cliff, Masaki Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mtemvu (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya wageni kutoka Chuo Kikuu cha Buffalo Marekani wakipata mlo wa usiku. Ujumbe huo umepangiwa kuonana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na kutembelea baadhi ya shule na Hospitlai katika Jimbo la Temeke.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Ally kushoto) na wenzie wakipata chakula
Mtemvu akidadiliana jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya African Maraika, Fiona Barrelto (katikati)  na mkewe Mariam wakati wa hafla hiyo.
Mfanyakazi wa Hoteli ya Sea Cliff (katikati) akichangamsha hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Sea Cliff wakiiimba wimbo huku wakipiga makofi ikiwa ni moja ya sham rashamra ya hafla hiyo.
Wageni ambao ni wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Buffalo Marekani wakiwa wamesiamama walipokuwa wakitambulishwa kwenye hafla hiyo.
Mtemvu akielezea umuhimu wa ziara ya marafiki zake hao nchini.
Mwanafunzi Tyler Choi wa Chuo Kikuu ccha Bufalo akitoa shukurani kwa kuandaliwa hafla hiyo pamoja na kuahidi kudumisha urafiki uliopo na Mtemvu na Jimbo la Temeke kwa ujumla.
Barrelto ambaye ni mfadhili mkubwa katika sekta ya elimu Jimbo la Temeke, akielezea umuhimu wa kudumisha urafiki uliopo kati ya chuo hicho na Mtemvu (kushoto). Kulia ni Mke wa Mtemvu, Mariam ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalum Temeke.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...