Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(Shati la Kitenge) akifanya ukaguzi wa ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea jana Januari 07, 2014 Mjini Dodoma. Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza limepewa jukumu la kukarabati jengo hilo na kukamilisha kazi hiyo mapema mwezi Februari, 2014 kabla ya Bunge Maalum la Katiba kuanza.
Msimamizi wa mradi wa ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Injinia. Salum Omary(kushoto) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(Shati la Kitenge) hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ukarabati wa Jengo hilo unaoendelea(kulia shati la drafti) ni Kamishna wa Magereza, Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Injinia. Deonice Chamulesile ambaye ameongozana na Kamishna Jenerali Minja katika ukaguzi huo.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kibwana Kamtande(kushoto) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza alipofanya ukaguzi mradi wa ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana Januari 07, 2014 Mjini Dodoma. Wengine ni Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Mkoa wa Dodoma.
Baadhi ya Wafungwa wa Gereza Kuu Isanga, Dodoma wakisaidiana na mafundi kutoa nguvu kazi ya kusogeza vifaa vya ujenzi kama wanavyoonekana katika picha. Shughuli za ujenzi ni moja ya programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa wakati wanapokuwa wakitumikia vifungo vyao magerezani hivyo kuwapatia ujuzi mbalimbali pindi wamalizapo vifungo vyao waweze kupata ujuzi ambao utawasaidia wanapokuwa wamerejea katika jamii zao
Muonekano wa juu wa Jengo la Ofisi za Utawala za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo hivi sasa linafanyiwa ukarabati na Kikosi cha Ujenzi cha Jeshi la Magereza kilicho chini ya Shirika la Magereza. Ukarabati wa jengo hilo kama linavyoonekana katika picha unatarajiwa kukamilika mapema mwezi Februari 07, 2014 kabla ya Bunge Maalum la Katiba kuanza.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
No comments:
Post a Comment