Thursday, January 16, 2014

Ujumbe wa Algeria umepata nafasi ya kutembelea machimbo ya Tanzanite Mererani

 Mkurugenzi Mkuu wa Migodi katika Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria Bw. Bourroudj Mohamed Tawar (aliyenyoosha mkono) akiangalia mwamba uliotokana na masalia ya ndege aina ya flamingo, yanayozalisha Mbolea ya kupanda ya Minjingu. Mwenye koti jeupe ni  Mkuu wa uzalishaji wa kiwanda cha Minjingu Bw. Inyana Mwambete, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho  Bw. Tosky Hans na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Samaje.
 Mtaalamu wa madini katika machimbo ya Kampuni ya TanzaniteOne Mererani Bw. Damian Mansala akiueleza ujumbe  wa Algeria namna mitambo ya kupeleka wachimbaji ardhini na namna mtambo huo unavyosafirisha mchanga wa madini uliochimbwa na kuusambaza katika hatua  mbalimbali za uzalishaji wa madini ya Tanzanite.
 Meneja Mradi wa Kampuni ya TanzaniteOne Bw. Erenet Emmanuel Mtawali (mwenye kofia nyekundu) akiueleza ujumbe wa Algeria namna mitambo ya kusafisha na kuzalisha madini ya Tanzanite (haupo pichani) unavyofanya kazi.
Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Sameja akiuongoza ujumbe wa Algeria kuondoka katika uwanja wa ndege wa Arusha , mara baada ya kumaliza ziara Mkoani humo.
----
Ujumbe wa Algeria umepata nafasi ya kutembelea machimbo ya Tanzanite Mererani katika Kampuni ya TanzaniteOne ambapo walitembelea sehemu mbalimbali ikiwemo za uzalishaji, usafishaji, na uchongaji madini ya Tanzanite. Vilevile, wakiwa Mkoani Kilimanjaro walipata fursa ya kutembelea Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya kupandia cha Minjingu ambapo walijionea namna mbolea hiyo inavyozalishwa kwa kutumia masalia ya ndege aina ya Flamingo waliokuwepo eneo hilo miaka mingi iliyopita. 

Aidha, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea mbuga za wanyama katika bonde la ngorongoro ambapo wamehitimisha ziara yao nchini ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na nchi ya Tanzania katika sekta za gesi, mafuta,umeme na madini.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...