Wednesday, January 22, 2014

Ona Jinsi Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa Alivyopokelewa Kwa Shangwe Katika Ofisi Za Wizara Hiyo

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. M.Tarishi (kushoto), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa (Katikati) na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Kulia) wakibadilishana mawazo baada ya mkutano wao na watumishi wa wizara ya maliasili na utalii.
   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Wanyamapori, Profesa Kidegesho.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa akiongea na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI mpya katika Wizara ya Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu na Naibu Waziri mpya mh. Mahmood Mgimwa wapokelewa kwa shangwe makao makuu ya wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam.

 Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya mapokezi ya Mawaziri wake wapya leo Jumanne 21 Januari 2014, ambapo watumishi waliopo Makao Makuu ya wizara wamepata fursa ya kukutana na kufanya maongezi na mawaziri hao. 

Mapokezi hayo yanafuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzanaia Mhe. Jakaya Kikwete.
 


Naibu Waziri Mhe. Mahmood Mgimwa amewaahidi wafanyakazi wa Maliasili na Utalii kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kuleta maendeleo ambayo wananchi wanayategemea kutoka katika Wizara hii. 

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewakikishia wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi ili kuweza kuifanya Wizara kuongeza pato la Taifa kupitia Utalii. 

Aidha, Mhe Nyalandu amewaasa watumishi wote kudumisha amani na upendo katika maeneo yao ya kazi ili kujenga mazingira mazuri ya kazi na kuongeza ufanisi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...