Kada wa CCM Frederick Mwakalebela na Simon Belege kushoto wakiwa katika mkutano huo
Na Francis Godwin Blogu
CHAMA cha mapinduzi ( CCM) wilaya ya Iringa mjini kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli jimbo la Iringa mjini huku katibu wa CCM wilaya hiyo Hassan Mtenga amemtaka mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi kumbana mbunge mchungaji Peter Msigwa ili kuonyesha mamilioni ya shilingi ambayo anadai yalitolewa na mfanyabiashara Sabodo kwa ajili ya kusaidia maji wananchi wa jimbo la Iringa wakiwemo wa Nduli. Mbali ya katibu huyo kumwagiza meya kufuatilia fedha hizo ili kujua kazi ambayo zilifanya pia Meya Mwamwindi ameueleza umati mkubwa wa wananchi waliofika katika mkutano huo kazi chache ambazo anazitambua alizozifanya mbunge Msingwa kwa miaka yake miwili akiwa mbunge.

Imedaiwa mfanyabiashara Sabodo mwaka jana alinukuliwa na vyombo vya habari akijitolea fedha za uchimbaji wa visima vya maji kwa wabunge wote wa majimbo wa CHADEMA kama njia ya kumaliza kero ya maji majimboni mwao ila hadi sasa jimbo la Iringa mjini eneo la Kigonzile kata hiyo ya Nduli wananchi wake wanashida kubwa ya maji.
Mwamwindi alitaja kazi hizo kuwa ni pamoja na kugawa mipira kata zote 16 isipo kuwa Nduli,kupeleka vitanda visizo chakavu katika Hospitali ya wilaya ya Iringa mjini (Frelimo) vitanda ambavyo hadi sasa havitumiki ,pamoja na kutoshindwa kushiriki vikao vya baraza la madiwani kwa miaka miwili kabla ya kulalamikiwa na kazi nyingine ambayo amekuwa akiifanya ambayo haina faida kwa wana Iringa ni kupigania ujangili wa Twiga na Tembo hali akijua jimboni kwake hakuna hifadhi ya wanyama. Pia Mwamwindi alipongeza jitihada zinazofanywa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kwa kujenga kituo cha polisi kusaidia ufunguzi wa Hospital ya wilaya , kusaidia kusomesha yatima, kuwezesha wanawake kiuchumia na kazi nyingine nyingi.
Hata hivyo alisema mbali ya kuwa katika mfuko wa jimbo kuna kiasi cha Tsh milini 30 ambazo zimetolewa na Rais Jakaya Kikwete ila wajumbe wa mfuko huo wamekuwa wakishindwa kukutana kutoa maamuzi juu ya fedha hizo kutokana na mbunge kuonyesha kuwazunguka na kugoma kukaa vikao.
Mwamwindi alisema kuwa serikali ya CCM katika kata hiyo ya Nduli pekee imefanikisha kusogeza maendeleo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja katika kijiji cha Kigonzile pamoja na kufikisha usafiri wa daladala ambapo toka nchi ipate uhuru wananchi hao kwa sasa wanapata usafiri , pia kwa nduli ujenzi wa shule ya sekondari pamoja na kupeleka mradi kubwa wa maji unaogharimu zaidi ya Tsh milioni 70 mradi ambao mbunge wao amekuwa hauungi mkono kutokana na kususa siku ya uzinduzi.
Huku kwa upande wake aliyekuwa mshindi wa kura za maoni katika mchakato wa ndani ya CCM mwaka 2010 Frederick Mwakalebela akiwataka vijana na wananchi wa kata ya Nduli kumchagua mgombea udiwani wa CCM Bw Benitho Mtove kuwa ndie atakayefanikisha maendeleo ya jimbo la Iringa na kata ya Nduli.
Akihotubia huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliofika katika mkutano huo Mwakalebela alisema bado anaheshimu jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya CCM chini ya rais Kikwete na kuwa ili kasi ya maendeleo iendelee kuwepo wananchi wa Nduli hawana budi kuchagua CCM na sio kuchangua mpinzani.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu aliwataka wananchi wa Nduli katika kumuenzi diwani aliyefariki duni Idd Chonanga kutobabaika na kauli za Msingwa na badala yake kuchagua diwani wa CCM.
Hata hivyo mgombea huyo wa udiwani Bw Mtove ambae hakutaka kumzungumzia mbunge Msigwa wala mgombea wa Chadema udiwani katika kata hiyo ,alisema anahakika atafanya kazi ya kuwatumikia wananchi wa Nduli na kuomba tarehe 9 kumpa kura zote za ndio.
No comments:
Post a Comment