Monday, January 20, 2014

13 WAFARIKI KATIKA AJALI ISUNA, SINGIDA

 Hali ilivyokuwa baada ya ajali hiyo.
Habari zilizotufikia sasa hivi kutoka Singida zinasema watu 13 wamefariki dunia baada ya kutokea ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Isuna mkoani humo.
Habari zinasema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Noah na lori ambayo namba zake za usajili hazikupatikana mara moja. Watu 13 waliofariki walikuwa katika Noah iliyokuwa ikitokea Itigi na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida. 


Baada ya ajali hiyo, dereva wa lori na msaidizi wake walitokomea kusikojulikana.

No comments:

RAIS SAMIA AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA JUMUIYA YA MADOLA IKULU DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 15 Aprili 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe...