Wednesday, January 08, 2014

Muda Mfupi Baada ya Mahakama Kuu Kuamuru chombo chochote cha CHADEMA, hakitaruhusiwa kujadili suala la uanachama wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini -Chadema Zitto Kabwe hadi kesi yake ya msingi aliyoifungua mahakamani itakaposikilizwa.

 Huyu mwenzake naye pia wa Chadema  akiwa na bango na kumfagilia Zitto
Wafuasi wa Chadsema wanaouunga mkono Zitto wakiwa wameunganisha mabango yao kuonyesha jina la Zitto mbele  ya mahakama kuu.
 Wafuasi waliojita,mbulisha kuwa wa Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe  wakihamasika nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, wakati ilipokuwa ikisubiriwa hatma ya kesi aliyofungua mbunge huyo dhidhi ya chama chake ,Kesi hiyo inaendelea leo baada ya kuahirishwa jana
 Wafuasi wanaodaiwa kuunga mono uongozi wa Chadema nao wakiwa katika kundi lao mbele ya jendo la mahakama kuu wakati ikisubiriwa hatma hiyo.
  Kinana anayedaiwa kuwa mfuasi wa Chadema akiwa amedakwa na polisi akidaiwa ni mamluki waliokodiwa kufanya fujo mahakamani hapo
 Wakili wa Zitto akisindikizwa na wafuasi wa mbunge huyo baada ya kesi kuahirishwa jana
  Wafuasi wa Chadema wanaounga mkono uongozi (kushoto) na wale wanaomuunga mkono Zitto (kulia) wakitoka mahakamani huku kila kundi likiandamana kivyake kubeza kundi lenzake
  Mwanzoni watumishi wa mahakama Kuu wakiweka vizuizi kuimarisha usalama mbele ya mahakama kuu
  Mmoja wa mashabiki wanaounga mkono uongozi wa Chadema (kushoto) akisakamwa baada ya kwenda upande wa wale wanaomuunga mkono Zitto
 
  Wafuasi wa Chadema wanaounga mkono uongozi wakibishana jambo na polisi nje ya mahakama, huku mfusi wa CUF (kulia kabisa) akiwaunga mkono wafuasi hao wa Chadema bila shaka kama mwalikwa.
Polisi wenye mbwa mkali hawakucheza mbali.Picha Zote na Bashir Nkromo
---
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,  imeamuru Kamati Kuu ya CHADEMA kutojadili uanachama wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Amri hiyo imo katika uamuzi wa Jaji John Utamwa, ambaye amekubali hoja za upande wa Zitto, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Alisema kwamba hoja zake zimekidhi matakwa ya kisheria ya kutolewa kwa zuio la muda la kutojadiliwa kwa uanachama wake.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Utamwa alisema Kamati Kuu ya chama hicho au chombo chochote cha CHADEMA, hakitaruhusiwa kujadili suala la uanachama wa Zitto hadi kesi yake ya msingi aliyoifungua mahakamani itakaposikilizwa.

Zitto amefungua kesi dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chama hicho na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa, akiiomba Mahakama itoe zuio hilo, hadi atakapokata rufaa ya kupinga uamuzi uliomvua uongozi wa chama.

Aidha anaiomba Mahakama imwamuru Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Slaa ampe nakala zinazotoa sababu za uamuzi wa kumvua uongozi katika kikao kilichofanyika Novemba 22 mwaka jana, ili akate rufaa katika Baraza Kuu la Chama.

Katika uamuzi wake Jaji Utamwa alisema kwa mujibu wa Sheria ili Mahakama itoe zuio, ni lazima katika suala la msingi kuwe na mtu ambaye atapata madhara ambayo hayatarekebishika.

Alisema katika ombi la Zitto, amekidhi matakwa ya kisheria, kwa kuwa zuio hilo lisipotolewa na akavuliwa uanachama, atapoteza nafasi ya ubunge na kushindwa kuwatumikia wananchi waliomchagua na pia atapoteza nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge wa Kamati ya Kudumu ya  Hesabu za Serikali.

Jaji Utamwa alisema endapo Zitto atavuliwa uanachama kabla hajapewa haki ya kusikilizwa, atapata madhara makubwa ambayo hayarekebishiki hata kama uchaguzi utafanyika tena.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...