Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Goodluck Ole Medeye(kushoto) akimkabidhi ofisi Naibu Waziri mpya katika Wizara hiyo George Simbachawene (Kulia)leo kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete hivi karibuni. Picha/ Clarence Nanyaro/Ardhi GC
Friday, January 31, 2014
MAKAMU MWENYEKITI WA CCM PHILIP MANGULA AWASILI MKOANI MBEYA
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya tayari kwa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM zinazofanyika jumapili kwenye uwanja wa Sokoine mkoani humo, Katika sherehe hizo Mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Rais Dr. Jakaya Kikwete. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYAMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi. Siasa na Uenezi wakati alipowasili katika ofisi za CCM mkoa wa Mbeya leo katikati ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey ZambiMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na Abdallah Bulembo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa.Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya.Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akiongozana na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi kushoto na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi. Siasa na UeneziMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangulaakisaini kitabu cha wageni
RAIS AONDOKA KWENDA NCHINI INDIA KWA ZIARA RASMI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo wa India anyefanyia kazi Zanzibar wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake (katikati) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shei,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi Mdogo wa India anyefanyia kazi Zanzibar wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake, pichani akipeana mkono na Brigedia Jenerali Sheikh Sharif Othman .[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Viongozi mbali mbali katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipokuwa akiondoka kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuelekea nchini India kwa ziara Rarsmi akiwa na ujumbe wake,[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]
DK ASHA ROSE MIGIRO AITEMBELEA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA
Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro (kushoto) akipokea maua kutoka kwa Afisa Tawala wa Tume Bi. Suzan MagotiMh. Migiro akisalimiana na Mwandishi Mkuu wa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Caritas MushiWaziri wa Katiba na Sheria Mhe. Asha Rose Migiro akizungumza wakati wa kikao chake na uongozi wa TumeKikao cha pamoja baina ya Mhe Waziri wa Katiba na Sheria na Uongozi wa TumeMwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanazania Mh. Jaji Aloysius Mujulizi akimpokea WazIri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro alipotembelea ofisi za TumeMwenyekiti wa Tume Mhe. Jaji Aloysius Mujulizi akizungumza wakati Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Asha Rose alipoitembelea TumeWashiriki wa KikaoSehemu ya Watumishi na ugeni wa Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha pamojaKatibu Mtendaji wa Tume Bi. Winfrida Korosso akiwasilisha taarifa fupi ya Tume kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Asha Rose Migiro
KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA WATEMBELEA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO
Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Mhe. William Mganga Ngeleja akizungumza na watendaji na menejimenti ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakati Kamati yake walipotembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kukagua utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu.
Picha na Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dk. Philip Mpango akizungumza wakati wa Ziara hiyo.Wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala walipotembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kukagua utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu.Wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala walipotembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kukagua utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu.
WAZIRI MKUU WA FINLAND ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe(kushoto), akimtabulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka(aliyevaa tai nyekundu) kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen, wakati Waziri Mkuu huyo alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), jana asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe akitoa ufafanuzi wa namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen(wa tatu kutoka kushoto) , wakati alipotembelea Mamlaka hiyo jana asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka. Kulia kwa Waziri Mkuu wa Finland ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na kushoto kwa Waziri Mkuu huyo ni Waziri wa Niashati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Madeni Kipande, akitoa maelezo ya awali ya namna ambavyo Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka hiyo jana asubuhi kuangalia namna Mamlaka hiyo inavyofanya kazi. Aidha, Waziri Mkuu huyo alitembelea Gati namba 1-7.Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akichangia mada wakati wa Mkutano na Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) jana asubuhi kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo.Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo. Nyuma ya Waziri Mwakyembe ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
MWILI WA SHEKH WA MKOA WA MARA WAWASILI UWANJA WA NDEGE MUSOMA
NDEGE ILIYOBEBA MWILI WA MAREHEMU SHEKH ATHUMANI MAGEE
MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIELEKEA KWENYE NDEGE KUONGOZA WAOMBOLEZAJI
RUBANI WA NDEGE AKIELEKEZA NAMNA YA KUTOA JENEZA LENYE MWILI WA MAREHEMU
MKUU wa mkoa wa Mara Mheshimiwa John Gabriel Tuppa ameongoza maelfu ya Wananchi wa Mji wa Musoma kupokea mwili wa Shekh wa Mkoa wa Mara Athumani Magee aliyefariki dunia usiku wa januari 28 katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kugua kwa muda na mrefu na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Musoma wakiusubili mwili wa shekh Magee wamesema wamepata pigo kubwa kutokana na msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza masuala ya dini.
Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa kesho kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.
INNAH LILLAH WAINNAH ILLAH RAJIUUN
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA SHOMARI BINDA
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA SHOMARI BINDA
WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII, WATEMBELEA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII, RUNGEMBA IRINGA. RUNGEMBA
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (mb.) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa,Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii leo wametembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa. Lengo la ziara hii ni kukagua utekelezaji wa shughuli za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika utoaji wa Mafunzo ya Maendeleo ya Jamii kupitia chuo hiki. Katika ziara hii, wajumbe wa kamati walipata fursa ya kupokea taarifa ya chuo na kutembelea maeneo / miradi mbalimbali ya chuo.Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe.Saidi Mtanda (Mb.) wakikagua maeneo / miradi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na kutoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, katika baadhi ya maeneo yenye kuhitaji maboresho.Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Kati) pamoja na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba, (Kulia, mwenye nguo ya kahawia) Bibi Santina Mbata wakiwapitisha Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Majengo / miradi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba.
UNIC YAENDELEA KUTOA MAFUNZO YA MATESO YA KAMBI ZA WAYAHUDI
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.
Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.
“Ni muhimu kutoa mafunzo kwa vijana wakitanzania wa shule za msingi na sekondari ili wajue kwamba tofauti za rangi na za kidini hazina nafasi ya kutugawa kama binadamu,” amesema Nkhoma.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Diamond na Mlezi wao wakimsikiliza Bi. Ledama (hayupo pichani).
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto.
Alisisitiza kwamba mauaji na mateso ya Auschwitz yalipoteza mamilioni ya watu wasio na hatia na mafunzo haya yanaonyesha chuki na ubaguzi dhidi ya wayahudi na chuki za aina nyingine yoyote hazina nafasi katika ulimwengu wa leo.
Nkhoma amesema kwamba binadamu wote ni sawa na tofauti za kipato au dini au rangi haziwezi tena kujenga chuki dhidi ya binadamu wengine kwa sababu wote kama binadamu tuna haki sawa mbele za mungu.
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond jijini Dar es Salaam, wakifuatilia sinema maalum ya mauaji ya kambi za mateso ya wayahudi mwaka 1933.
Wakati huo huo, ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto amesema aliona makambi ambako wayahudi, waroma, wasinti, mashoga, wafungwa wa kivita na watu wenye ulemavu walitumia siku za mwisho katika hali ya kinyama.
“Umoja wa Mataifa ulianzishwa kuzuia kila aina hii ya fazaa kutokea tena, lakini bado misiba kuanzia Cambodia hadi Rwanda mpaka Srebrenica inaonyesha kuwa sumu ya mauaji ya kimbari bado inatiririka,” ilisema taarifa hiyo.
Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond wakisoma baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa.
UBALOZI WA CHINA NCHINI WASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO WA MOROGORO
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Youqin. akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi misaada hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali Sylivester Rioba akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali kutoka kwa Balozi wa Mhe. Lu Youqin.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Eliphace Marwa-Maelezo
Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kushirikiana na makampuni ya watu wa China nchini wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko mkoani Morogoro toka kwa Mhe. Lu Youqing ,vyenye thamani ya sh. milioni 30.
Msaada huo umetolewa na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.Lu Youqing na ulikabidhiwa kwaMkurugenzi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Jenerali Sylivester Rioba akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali amesema kuwa anaishukuru Serikali ya China kwani imekuwa mstari wa mbele pale Tanzania inapopata maafa mbalimbali.
Aidha Luteni Jenerali Rioba aliongeza kuwa mafuriko hayo ya aina yake hayajawi kutokea yalianzia milima ya Kilosa na Mvomero na kupelekea kufurika kwa mto Mkundi.
“Mheshimiwa Balozi mvua hizi zilikuwa kubwa ambazo hazijawahi kutokea wilayani Mvomero na kupelekea kuharibu daraja la Dumila ambalo ndiyo kiunganishi cha Mkoa wa Morogoro na Dodoma,” alisema Luteni Jenerali Rioba.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe.Antony Mtaka akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema kuwa mamia ya nyumba ikijumuisha madarasa, majengo ya mahakama ya mwanzo, mashamba na barabara zimeharibiwa vibaya na mafuriko hayo.
“Kwa niaba ya Serikali napenda kushukuru Serikali ya China kupitia Mhe. Balozi Lu kwa msaada huu na ningependa kuahidi kuwa msaada huu utawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa, ”alisema Mhe. Mtaka.
Kwa upande wake Balozi wa china ametoa pole kwa waathirika wa mafuriko na kusema kuwa watu wa Jamhuri ya China wako pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.
“China na Tanzania ni marafiki wa muda mrefu hivyo kampuni ya ujenzi ya CCECC ilichukua hatua za haraka katika kushiriki ujenzi wa daraja hilo kwa kushirikiana bega kwa bega na ndugu zao Watanzania kwa kufanya kazi usiku na mchana na kumaliza ujenzi huo kwa muda wa siku mbili,” alisema Balozi Youqing.
Ubalozi wa China kwa kushirikiana na makampuni ya China nchini umetoa vitu mbalimbali ikiwemo Chakula, mashuka, madawa na maturubahi ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa waathirika hao wa mafuriko mkoani Morogoro.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...