Friday, December 21, 2012

Wasanii Wakongwe wa Muziki wa Dansi Wamtembelea Rais Jakaya Kikwete na Kumshukuru kwa kuwajali


Rais Jakaya kikwete akijadiliana jambo na Mwanamuziki Mkongwe kutoka Bendi ya Kilimanjaro Band Wana Njenje Bw Waziri Ally Muda mfupi baada ya ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu kumtembelea  Ikulu jijini Dar es salaaam leo
 Mr Waziri Ally kutoka bendi ya kilimanjaro Band wana  Njenje akitoa salaam za shukrani na pongezi kwa niamba ya  ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam leo
Rais jakaya kikwete akimshukuru Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Dansi nchini King Kiki
 Picha juu Rais jakaya kikwete akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam leo
--
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Desemba 21, 2012 amepokea ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam kwa kuwajali wasanii wa aina zote na hata kuamua kutoa tuzo kwa wasanii
ambapo mwaka huu amewatunuku Muhidin Maalim Gurumo na Hayati Marijani Rajabu.Picha na IKULU

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...