Pichani
kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akiwakaribisha
wageni wake, akiwemo mwanamuziki nyota wa dansi ndani ya kundi la Wenge
BCBG,kutoka nchini DRC-Congo, JB Mpiana (pichani kati) kwenye hafla fupi
ya chakula cha usiku iliyofanyika kwenye kiota cha maraha cha Escape
2, kilichopo Kunduchi jijini Dar, hafla hiyo pia ni sehemu ya muendelezo
wa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 13 ya Clouds FM tangu
kuanzishwa kwake hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga akiwakaribisha wageni wake na
kuzungumza nao machache na kuhakikisha wanapatiwa chochote kitu.
Mkurugenzi
wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimtambulisha mke wake Johayna
Kusaga (ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Prime Time
Promotions Ltd) kwa Mwanamuzik JB Mpiana na kwa wageni wengine waliofika
kwenye hafla hiyo ya chakula cha pamoja.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimkaribisha mgeni wake JB Mpiana kwenye chakula
Pichani
ni baadhi ya Washiriki wa shindano la Miss East Afrika 2012 ambao pia
walialikwa kwenye chakula cha pamoja ndani ya kiota cha maraha cha
Escape 2,kilichopo Kunduchi jijini dar.
Washiriki wa shindano la Miss East Afrika wakiwa katika picha ya pamoja
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Cassim akitumbuiza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali
Boniventure
Kilosa a.k.a Dj Venture alikamata mashine na kuangusha ngoma kali
zikiwemo za Kinaija,abazo wageni wengi walionekana kuburudishwa nazo
vilivyo.
Washiriki wa shindano la Miss East Afrika 2012 wakijiachia vilivyo kwa mikato ya ngoma iliokuwa ikiangushwa na Dj Venture.
Joseph
Kusaga a.k.a Boss JOe akizungumza na baadhi ya wasanii mahiri wa muziki
wa kizazi kipya,Ay na Mwana FA ndani ya hafla fupi ya chakula cha usiku
kulichoandaliwa kwa ajili ya wageni.
Wadau nao walikuwepo.Mdau wa MJ FM pamoja na Andrew Kusaga wakishoo love.
Wafanyakazi mbalimbali kutoka Clouds Media Group walikuwepo pia |
Kuserebuka kama hivi pia kulikuwepo .
Mtangazaji wa Clouds TV,Ben Kinyaiya akifanya mahojiano mafupi na mwanamuziki mkongwe wa dansi,Ndandaa Kossovo.
Dj Venture na mshkaji wake wakivuta pumzi.
Mmoja
wa Wakurugenzi wa Prime Time promotios,pichani kulia Godfrey Kusaga
akibadilishana mawazo na Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Jahazi cha
Clouds FM,Ephrahim Kibonde huku wakiangusha moja moja.
Mazungumzo ya hapa na pale pia yalikuwepo.
Pichani shoto ni Dj Bon Love,Balozi,Godliva pamoja na Ephraim Kibonde wakishoo love.
No comments:
Post a Comment