Rais azindua nyumba za gharama nafuu Kibada

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa PMU NHC, Khamis Mpinda
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wenyekiti wa Tamico NHC, Daniel Nkya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi NHC, Kesogukewele Msitta na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa NHC baada ya kuzindua mradi wa nyumba za garama nafuu NHC Kibada.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete amezindua mradi huu wa gharama nafuu rasmi leo (tarehe 13 Desemba, 2012) na Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania. Uzinduzi wa Mradi huu wa Kibada, unaashiria pia kuanza kwa miradi ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu inayotekelezwa na Shirika katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri za Wilaya hivi sasa.

Mradi huu uliopo  eneo la Kibada, Kigamboni – Dar es Salaam, takribani kilomita 10  kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam, una nyumba za gharama nafuu zipatazo 296.

Pia Mradi unatarajiwa kuboresha maisha ya wanunuzi wa nyumba hizi kwani upo karibu kabisa na jiji na kwamba mnunuzi anaweza kwenda kazini bila kutumia gharama kubwa ya usafiri wa gari.  Aidha, nyumba zitapokamilika zitakuwa ndani ya uzio kwa ajili ya usalama wa wakaazi wake  na kuna maegesho ya magari ya kutosha.

Nyumba  290 tu zinazouzwa ambapo zipo nyumba za aina mbili ambazo ni nyumba ya vyumba vitatu na ya vyumba viwili. Nyumba ya vyumba vitatu ina ukubwa wa  mita za mraba 70  huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na ukubwa wa mita za mraba 56.

Mojawapo ya nyumba za Kibada

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi mradi wa ujenzi wa nyumba 290 za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) maeneo ya Kibada, Kigamboni, wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es salaam leo December 13, 2012 . Kushoto ni Mama Salma Kikwete, kulia ni Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye, anayefuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mhandisi Kesogukewele Msita , Mkurugenzi Mkuu Bw. Nehemia Mchechu,

Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa , Chumba kimoja kinachojitegemea kwenye nyumba ya vyumba vitatu, kila nyumba ina sebule na sehemu ya kulia chakula, ukuta unaotenganisha mipaka kati ya maeneo ya wakazi, jiko la nje, eneo la zahanati, eneo la kucheza watoto, eneo la shule ya chekechea na eneo la maduka.

Comments