Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila 'RAY C'
akimshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu aliompatia ikulu jijini
Dar es Salaam leo
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C (wa tatu kushoto), Mama
yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na Sarah Mtweve Dada
yake Ray C.Picha na Freddy Maro-IKULU-
--
Na Freddy Maro, Ikulu
Mwanamuziki wa
Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa
msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Rehema
aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah
Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu
atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.
Kwa apande
wake, Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya
mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili
ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa
na Rais.
No comments:
Post a Comment