Monday, December 17, 2012

Lowassa ashiriki harambee ya kanisa Akyeri Meru

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokelewa na viongozi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri, Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha kwa ajili ya kuongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa kanisa hilo, iliyofanyika leo Mkoani humo.

===========     =========   =========
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa amesisitizia tena kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni jambo la hatari kwa usalama wa nchi,wakati alipokuwa katika harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la kilutheri usharika wa Akyeri Meru mkoani Arusha, Mh lowassa ameonya kuwa suala hilo lisiposhughulikiwa haraka litasababisha hali ya hatari.

”tunashuhudia maandamano katika mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha pamoja na ajira.hali hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini kwetu.

huko nyuma niliwahi kusema kuwa makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie juhudi za serikali kutatua suala hilo”alisema Lowassa.

Lowassa ambaye katika harambee hiyo aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye na familia yake pamoja na marafiki zake wamechangia kiasi cha shilingi millioni 33.2.

Zaidi ya shilingi millioni 160 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana katika harambee hiyo.

Kwa upande wake askofu Akyoo wa jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa uchapakazi wake popote alipokuwa.”Wakati ulipokuwa Waziri Mkuu ukimsaidia rais tulishuhudia uwezo wako mkubwa katika kufuatilia majukumu yako”alisema na kuongeza kuwa Lowassa ni mtu wa ibada

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa tatu kushoto) akiongozana na Askofu wa Kanisha hilo la Lutherani usharika wa Akyeri, Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha,Askofu Akyoo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia muda mfupi kabla ya kuanza kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri, Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea ahadi ya mchango kutoka kwa mmoja wa wamini wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri, Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka kanisani hapo baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri, Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...