Tuesday, August 19, 2008

Mwalimu wa dini wake 86, watoto 170




DUNIANI kuna mambo. Mwalimu wa dini ya Kiislamu nchini Nigeria, Mohamed Bello Abubakar (84) pichani juu na wake zake,ambaye alimejitokeza na kutafuta rekodi ya kuwa na wake wengi, amewataka wanaume kutoiga tabia yake hiyo.

Bello Abubakar mwenye wake 86 pamoja na zaidi ya watoto 170 anaoishi nao katika mji wa Niger alieleza kupitia shirika la habari la BBC kuwa si vyema kwa wanaume wengine kuiga mfano wake, kwa kuwa uwezo alio nao ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

“Mwanauame mwenye wake 10 anaweza kupata kiharusi na kufa, lakini kwa nguvu niliyopewa na Allah nimeweza kuwadhibiti wake zangu 86 bila matatizo. Nimekuwa siwatafuti mimi, ila wamekuwa wakija wenyewe kwangu. Nimekuwa nikiamini kuwa Mungu ndiye amekuwa akiwaleta na sina namna zaidi ya kuwaoa,” alieleza.

Aliongeza kwa kusisitiza kuwa kwa kadiri ajuavyo, hakuna adhabu yoyote iliyoelezwa katika kitabu Kitakatifu cha Koran kwa kuwa na wake zaidi ya wanne na kwua uwezo wake unatokana na nguvu ya uponyaji aliyopewa na Mungu.

“Kwa uelewa wangu katika Koran Tukufu, haijaweka ukomo na inategemea nguvu zako na kadiri uwezo unavyoruhusu, Mungu hakueleza adhabu yoyote kwa mjwanaume mwenye wake zaidi ya wanne, lakini ameelez wazi adhabu kwa wabakaji na wazinzi,” alieleza alipokuwa akijibu swali kuhusu madai ya mamlaka za kiislamu nchini humo, kuwa mtu huruhusiwa kuwa na wake wasiozidi wanne, ambao atatakiwa kuhakikisha anawahudumia vyema.

Baadhi ya wanawake wa Bello, ambao wengi wao wana umri mdogo kuliko baadhi ya mabinti zake waleieleza kuwa walikutana na mwanamme huyo walipokwenda kwake kwa ajili ya kuomba usaidizi kutokana na maradhi kadhaa.

“Mara tu nilipokutana naye ugonjwa wa kichwa ulipotea,” alieleza Sharifat Belo Abubakar, mwanamke aliyekutana na Abubakar akuwa na miaka 25, wakati mwanamme huyo alipokuwa na miaka 74.

“Mungu alinieleza kuwa ni wakati wangu wa kuwa mke wake, Sifa kwa Mungu kuwa sasa imetimia na imekuwa mkewe. Nilipomuona mara ya kwanza niliapa kwua siko tayari kuolewa na mzee huyu na ulipofika wakati alinieleza wazi kuwa ni agizo kutoka kwa Mungu,” alieleza mwanamke mwingine, Ganiat Mohamed Bello, ambaye mama yake aliwahi kumpeleka kwa Bello Abubakar kwa ushauri alipokuwa akisoma shule ya Sekondari.

Aliongeza kuwa mara baada ya kumaliza shule alioana na mwanaume mwingine lakini muda si mrefu walitaliliana na alipokwenda kwa mzee huyo ambaye kwa kipindi cha miaka 20 ya uhai wake alikuwa akimuita baba hakuwa na namna zaidi ya kutekeleza agizo kutoka kwa Mungu.

“Kwa sasa ni mhongoni mwa wanawake wenye furaha duniani. Unapoolewa na mwanaume mwenye wake 86 unajua kabisa kuwa anaelewa namna ya kuwatunza,” alisisitiza.

Lakini maisha yake na wake zake hayana utaratibu maalum. Wake zake hao hawafanyi kazi na wanaishi zaidi ya wanne katika kila chumba na hana njia ya wazi kuhusu namna anavyoitunza familia yake kubwa. Hataki kueleza namna anavyoweza kupata fedha za kutosha kuweza kuwatumza wanawake hao.

Suala la kustaajabisha zaidi ni kuwa kamwe hajawahi kuwaruhusu wake zake wala watoto wake kutumia dawa ya aina yoyote wanapopatwa na maradhi mbali mbali kw akusema kuwa haamini iwapo kuna magonjwa kama Malaria duniani na kuwa wanapougua humweleza Mungu na Mungu huondoa maradhi yote.

Mmoja miongoni mwa wake zake, Hafsat Belo Mohammed alieleza kuwa watoto wake wanne walifariki, “waliugua na tukamweleza Mungu, Mungu akasema kwua wakati wao umefika.”

Lakini Bello Mohammed amekuwa akieleza kuwa Mtume Muhamad amekuwa akizungumza naye moja kwa moja na kumweleza mambo yote ambayo amekuwa akiyafanyia kazi.

Imeandaliwa na Andrew Msechu kwa msaada wa BBC

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...