Thursday, August 07, 2008
msiba wa Kapteni Mazula
MAELFU ya waombolezaji katikati ya wiki hii walijitokeza kwa wingi katika kanisa la katoliki usharika wa St Martha mikocheni kuusindikiza mwili wa marehemu Kapt George Mazula
Miongoni mwa sifa za Marehemu Kapt Mazula ni kutumia muda wa masaa 17,640 kuruka na ndege angani wakati wote wa uhahi wake alioishi hapa duniani.
Mbali na kukumbukwa katika mengi lakini pia Kapt Mazula atakumbukwa kwa tija na ufanisi katika kazi huku akiweka mbele masilahi ya taifa kuliko kutafuta faida zake binafsi.
Katika uhai wake aliweza kutumia masaa 3,300 kuendesha ndege ndogo yenye uwezo wa kubeba watu 19,masaa 7,340 watu wasiozidi 50 na zaidi ya masaa 7,000 ndege za B737.
Marehemu Kapt Mazula alipata matatizo ya mgongo ambayao yalisababisha apelekwe India kwa matibabu ,mnamo julai 8 mwaka huu aliweza kufanyiwa upasuaji na kupata nafuu jambo lililopelekea aweze kurudishwa nchini julai 20.
Hali yake iliendelea vizuri hadi julai 30 mwaka huu alipoanza kupata mtatizo ya pumu kabla ya roho yake kutwaliwa agosti mosi majira ya saa nne asubuhi akiwa nyumbani kwake.
Marehemu Kapt Mazula amewaacha watoto wake wawili Brayan Mazula na George -Junior mazula wanaoishi nchini marekani pamoja na mke wake Hariety Mazula.
Akisoma wasifu wa marehemu Kapt Mazula mtoto wake Georgejunior anasema marehemu alizaliwa mwaka 1949 katika eneo la bwiru mkoani Mwanza,yeye akiwa ni mtoto wa nne kuzaliwa kutoka kwa wazazi wake Arbogasti na Maria Mazula.
Anasema alisoma katika shule ya msingi Tabora, kabla ya kuhamia shule ya Kangululi wilayani ukerewe mkoani mwanza.
anasema katika masomo yake ya sekondari Marehemu Mazula alisoma katika shule ya musoma collegge na baadaye mwaka 1970 alijiunga na shule ya sekondari ya Aga Khan Boys kwa masomo ya kidato cha tano na sita.
Georgemazula anasema mwaka 1973 Kapt Mazula alijiunga na benki ya taifa ya biashara alikofanya kazi kabla ya kujiunga na chuo cha urubani Saroti kilichopo nchini Uganda. Habari hii ya Peter Edson na picha zote ni za Perez Mwangoka wa Mwananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment