Friday, August 15, 2008

Dereva wa daladala apiga mwanafunzi, azirai



KATIKA hali isiyo ya kawaida mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kisutu, Pili Jackson (17), jana majira ya asubuhi alijikuta akipata kipigo kutoka kwa dereva wa daladala, Michael Hassan (40) linalofanya safari zake Gongolamboto hadi Kivukoni, hali iliyomfanya azirai.

Dereva huo anayeendesha basi hilo lenye namba T156 ADV aina ya Toyota DCM, alijichukulia sheria mkono majira ya saa mbili asubuhi baada ya kutokea majibizano kati yake na dereva wakigombea kukaa eneo la mbele karibu na dereva ambapo hakukuwa na siti zaidi ya benchi dogo.

Mwanafunzi huyo alizimia kutokana na kipigo kilichomsababishia kudondokea siti moja wapo ndani ya gari hilo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akielezea tukio hilo alisema lilitokea jana majira ya saa mbili asubuhi maeneo ya Ukonga Mombasa, baada ya mwanafunzi huyo kupanda katika daladala hilo baada ya kuzuiwa na kondakta, hali iliyosababisha majibizano kati yao habari na Festo Polea.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...