Friday, August 01, 2008

Kapteni Mazula afariki dunia


Rubani mkuu wa atc kepteni george mazula amefariki dunia nyumbani kwake mtaa wa nyumbu, mikocheni, dar leo asubuhi baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kupumua.

msemaji wa familia, dk. charles lugora, amesema kwamba marehemu kepteni mazula alikuwa nchini india kiasi cha wiki tatu zilizopita alikokwenda kupatiwa matibabu ya athma na ali;porejea alikuwa anaendelea vyema hadi hali ilipobadilika ghafla asubuhi ya leo ambapo alifariki dunia milango ya saa nne unusu asubuhi.

Dr. Lugora amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake na ratiba kamili itatolewa kesho.

marehemu mazula aliyefariki akiwa na umri wa miaka 59, ameacha mke na watoto wawili (brian na george). mtoto wake wa tatu, walter, aliuwawa huko marekani septemba 2006, ambapo yeye na mchumba wake vonetha nkya waliuwawa kikatili na watu wasiojulikana.

mola aiweke roho ya marehemu pahala pema peponi,

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...