Sunday, August 03, 2008

Jengo jipya ndani ya Dar


Jengo la Uhuru Heights limesanifiwa kuwa jengo refu nchini mahsusi kwa ajili ya biashara na makazi. Kivutio hicho cha jengo kimebeba nembo ya mwenge wa uhuru ambao uliwekwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro

Jengo hilo la Uhuru Heights ni mradi muhimu kwa ajili ya kuifanya mitaji ya biashara na lipo sehemu nzuri kwenye Barabara ya Bibi Titi Mohammed katikati ya jji eneo la Upanga na Oyster Bay. Jengo hili litajengwa mbele ya bahari na litaweza kutoa fursa kwa watu kutazama na kupata upepo wa bahari ya Hindi na litakuwa na vifaa vilivyotengenezwa kwa ubora unaokubaliaka duniani.

Eneo litakapojengwa ni zuri na litavutia kibiashara. Ghorofa tano ndani ya jengo zitakuwa ni kwa ajili ya ofisi zenye ukubwa tofauti. Usanifu wa jengo na umaliziaji wa hali ya juu kutawezesha na kukidhi uendeshaji wa shughuli kama vile kuunganishwa na Intaneti iliyo na kasi kubwa, maegesho na ulinzi kwa saa 2.

Jengo hili litakuwa na ghorofa 25 litakuwa ni eneo la kuvutia, likiwa na burudani na mambo mengine ya kuvutia katika maisha ya jamii. Duka la nguo za mitindo yaaina mbalimbali litakuwa kwenye mwanzo wa jengo chini na kwenye ghorofa ya kwanza na litaonyesha mitindo mbalimbali inayopongoza kwa ubora duniani. Ghorofa ya pili itakuwa na mgahawa ambao utakuwa ni wa kipekee utakaokuwa na mchanganyiko wa vyakula kutoka tamaduni mbalimbali na utahudumia wateja kutoka mataifa mbalimbali sanjari na ukumbi mkubwa wa chakula.
Ukumbi wa burudani utakuwa na eneo la michezo mbalimbali ya watoto na ukumbi wa michezo.

Kwenye maeneo ya makazi ya jengo hilo kutakuwa na bwawa la kuogelea na sehemu ya kufanyia mazoezi ya viungo (gym) kwa ajili ya wanawake na wanaume, eneo lamichezo kwa ajili ya watoto na ukumbi wa sherehe ambao unaweza kuchukua watu 100 hadi 120

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...