Washiriki wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Uwanja wa Mpira wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi aliyazindua maonesho hayo huku akiwataka madereva nchini wawe makini kwa kufuatia sheria za barabarani ili kuepuka ajali. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”.
Waendesha pikipiki (bodaboda) na baiskeli nao pia walishiriki kikamilifu katika uzinduzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Kiwanja cha Mpira cha CCM Kirumba, jijini Mwanza jana. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”
Polisi kutoka Trafiki Makao Makuu jijini Dar es salaam, Dumu Mwalugenge, akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto), namna ajali barabarani zinaweza kuepukika endapo watumiaji barabara watakuwa waangalifu kwa kufuata sheria za barabarani. Waziri Nchimbi aliyazindua maonesho hayo ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani katika Kiwanja cha Mpira CCM Kirumba jijini Mwanza jana. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akiwa amevaa jaketi pamoja na kofia ngumu ambapo mavazi hayo huwa yanavaliwa wakati ya uzimaji wa moto. Waziri Nchimbi alivaa mavazi hayo wakati alipokuwa ndani ya banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika maonyesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo aliyazindua jijini Mwanza jana. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimpa cheti Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima kwa mchango wake aliouonesha katika kusimamia mapambano ya kutokomeza ajali za barabarani nchini. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa Kitaifa jijini Mwanza jana. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo na kulia ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP Mohamed Mpinga. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (watano kutoka kushoto), Naibu Waziri wa wizara hiyo na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (katikati) pamoja na maafisa usalama barabarani na wadau wa usalama barabarani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo Kitaifa yamezinduliwa na Waziri Nchimbi, jijini Mwanza jana. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KUTOKA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment