WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya
---
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya amesemwa Tanzania itafikia maendeleo ya hali ya juu ifikapo mwaka 2025 hadi mwaka 2030 ikiwa watu watafanyakazi kwa upendo, uzalendo na kujiamini.
Aidha Profesa Mwandosya amesema kwamba Serikali inajitahidi kufikisha huduma zake kwa karibu na wananchi, licha ya kuwepo kwa changamoto za kielimu na miundombinu, lakini mambo mengi yanafanyika,hivyo wenye macho wanaona.
Kauli hiyo imetolewa leo na Profesa Mwandosya wakati hafla fupi ya kukabidhi gari aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya Sh. milioni 38 iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dares Salaam.
“ Mimi nina matumaini makubwa na nchi yetu ifikapo mwaka 2025 hadi 2030 tutakuwa ni nchi yenye watu wenye kipato cha kati.Pia ifikapo mwaka 2050 nchi yetu itakuwa imeendelea hakutakuwa na mtu mwenye kipato cha kati wala cha chini kama ilivyo nchi ya Singapore,” alisema Profesa Mwandosya.
Profesa Mwandosya aliongeza kuwa gari hilo ni moja ya juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa huduma zake zinaifikia jamii kila mahali hususan kwenye maeneo ya vijijini.
“Serikali inajitahidi kufikisha huduma zake mfano katika sekta ya elimu kuna mambo mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika ikiwemo katika sekta nyingi kama vile kwenye nishati gesi tunakwenda vizuri. Tukisimamia vizuri rasilimali zetu ,basi hata huduma tutazifikisha vizuri kwa wananchi,” alisisitiza.
“ Kila mtu duniani anasema Tanzania inapiga kasi katika kuwaletea maendeleo wananchi . Mimi nadhani hatutarudi nyuma. Wale wanaopiga kelele hautajafanya kitu ,lakini mwenye macho wanaona,” alisisitiza Profesa Mwandosya.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Charles Pallangyo akizungumzia kuhusu gari hilo alisema litasaidia kuhimarisha huduma za chanjo katika halimashauri hiyo na kupunguza vifo vya wakinamama wajawazito na watotowenye umri wa chini ya miaka mitano ili kutimiza malengo ya millinea ya namba 4na 5 ifikapo mwaka 2015.
Naye Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando alisema nchi hivi sasa imefikia wastani wa asilimia 92 katika huduma za chanjo kutoka asilimia 90 ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga aliishukuru wizara hiyo kwa msaada huo ,ambapo alisema gari hilo litatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuinua kiwango cha huduma hiyo kwenye eneo hilo.
No comments:
Post a Comment