Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalimu Seif Sharif Hamadi akisisitiza kitu katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar jana.
Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim. Seif Sharif Hamadi akiwatubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wakishangiria katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar jana.
Baadhi ya waandishi wa Habari mbalimbili wakichukua matokeo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya kibanda maiti Mjini Zanzibar jana.
---
Na Khadija Khamis na Riziki Salum – Maelezo Zanzibar 22/09/2013.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalimu Seif Sharif Hamadi amelaani vikali vitendo vya hujuma vinavyofanywa na watu wasiojulikana kwa kuwamwagiwa tindikali watu wasio na hatia akiwemo Padri hapa Zanzibar .
Alisema kuwa vitendo hivi havivumiliki na Jeshi la Polisi wafanye kazi zao kitaalamu na kuweza kuwakamata wahusika ili wafikishe kwenye vyombo vya sheria.
Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu wa CUF huko katika Uwanja wa Kibanda Maiti wakati akiwahutubia wananchi katika Mkutano wa hadhara .
Aidha alilitaka Jeshi la Polisi wanapotoa maelezo yao kwa vyombo vya Habari waweze kutumia lugha nzuri katika kuwapa watu habari juu ya matokeo mbalimbali yanayotokea hapa nchini
Sambamba na hayo Katibu Mkuu huyo amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kutotia saini Mswada wa Marekebisho ya Rasimu ya Katiba kwani kuna baadhi ya mambo yameingizwa Bila ya kushirikizwa upande mmoja wa Muungano
“ Rais Kikwete alikuwa na nia nzuri tu kwa kuitangaza azma yake ya kutugwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika mwaka 2014 lakini kuna baadhi ya watu wachache wasiyoitakia mema Zanzibar”,alisema Maalim Seif.
Alifahamisha kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda alimuandikia barua rasmi Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idi ili kiushirikiana kufanya marekebisho ya sheria vifungu sita vya rasimu ya katiba kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili kutoa maoni yake .
Alifahamisha kuwa vifungu vitatu vilionekana kuwa havitoi haki kwa Wazanzibar vikabadilishwa kwa kuwekwa sawa baada ya marekebisho hayo yakafanyika marekebisho mengine manane bila ya kushirikishwa upande wa pili wa Muungano jambo ambalo chama cha CUF hawakuliridhia.
Maalimu seif aliwapongeza wale wote walioshiriki kikamilifu katika mabaraza mbali mbali ya wilaya kwa kuweza kujadili rasimu na kupeleka maoni yao ya marekebisho ya katiba .
No comments:
Post a Comment