Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA), Profesa Penina Mlama
Veronica
Kazimoto – MAELEZO, Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Profesa Penina Mlama (pichani) kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari - MAELEZO leo, Uteuzi huo wa
Profesa Mlama unaanzia mwaka 2013 na unatarajia kumalizika mwaka 2016.
Prof.
Mlama ni Profesa wa Sanaa na Sanaa za Maonyesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Aidha
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ameteua
jumla watu 12 kuwa wajumbe wa BASATA kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia
mwaka huu.
Walioteuliwa
ni pamoja na wawakilishi wa Vyama na Asasi mbalimbali wa Baraza hilo ambao ni
Dkt. Vincensia Shule, John Kitime , Angela Ngowi, Dkt. Herbert Makoye, Erick
Shigongo na Alex Msama.
Wawakilishi
wengine ni pamoja na Juma Adam Bakari, Daniel Ndagala, Michael Kadinde na Joyce
Fisoo.
Wanaoingia
kwa mujibu wa nyadhifa zao ni Prof. Hermas Mwansoko na Katibu Mtendaji wa
BASATA.
Katika
hatua nyingine Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella
Mukangara amemteua Bwana Ghonche Materego kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya
Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Kabla
ya uteuzi huo Materego alikuwa amemaliza muda wake kama Katibu Mtendaji wa
Baraza la Sanaa la Taifa.
Wajumbe
wa Bodi hiyo walioteuliwa na Waziri Mukangara ni Dkt. Herbert Makoye, Prof.
Emanuel Mbogo, Dkt. Lucy Mboma, Prof. Hermas Mwansoko pamoja na Katibu Mtendaji
wa BASATA.
Wakati
huo huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
ameteua jumla ya watu 21 kuwa wajumbe wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)
kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.
Wajumbe
hao ni Dkt. Shani Omari, Prof. Yohana Msangila, Ester Riwa, Dkt. Issa Zidi,
Khadija Juma na Dkt. Martha Qorro.
Wengine
ni Mmanga Mjawiri, Razia Yahaya, Richard Mbaruku, Selina Lyimo, Keneth Konga,
Amour Khamis, John Kiango, na Shani Kitogo.
Wajumbe
wengine ni Ally Kasinge, Ahmed Mzee, Rose Lukindo, Shabani Kisu pamoja na Edwin
Mgendera.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo la BAKITA atachaguliwa na
wajumbe watakapokutana kwenye kikao chao cha kwanza.
No comments:
Post a Comment