Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo (kushoto) akimwonesha Daktari Feki, Alex Massawe.
Daktari feki aliyenaswa katika hosptali ya KCMC aliyetambulika kwa jina
Daktari feki aliyenaswa katika hosptali ya KCMC aliyetambulika kwa jina
la Alex Massawe akiwa amefungwa pingu mikononi mwake katika eneo
la hosptali hiyo.
Daktari Feki akisindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa hosptali ya KCMC kutoka katika moja ya wodi ambayo alikuwa 'akihudumia'.
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, jana ulimnasa 'Daktari Feki' aitwaye Alex Sumni Massawe (33).
Massawe alikamatwa saa 5:00 asubuhi ndani ya hospitali hiyo na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amepanga kumfanyia upasuaji wa ngozi, Makasi Tipesa ambaye anasumbuliwa na ugonjwa huo baada ya kukutana na mama yake na kumuahidi kumpatia huduma kwa malipo ya Sh. 200,000.
Habari zinasema kuwa kabla ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi wa kijana huyo, mkazi wa Manispaa ya Moshi, Pamvelina Shirima, alikutana na mtuhumiwa huyo katika baa moja maarufu iliyopo eneo la Dar Street (jina limehifadhiwa) na kumtaka ampe kiasi hicho cha fedha kwa madai zitatumika kuharakisha mwanaye wa kiume kufanyiwa vipimo vya upasuaji.
Ofisa Uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo, alisema kuwa daktari huyo aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo baada ya baadhi ya wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mtu ambaye amekuwa akijitangaza kwamba ni daktari.
No comments:
Post a Comment