Friday, November 27, 2026

WAZIRI KOMBO NA WAZIRI KAIRUKI WAPOKELEWA RASMI WIZARANI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, leo Novemba 27, 2026, wamepokelewa rasmi katika ofisi zao jijini Dar es Salaam, kufuatia kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mapokezi hayo yamewahusisha pia Naibu Mawaziri wa Wizara hizo, Mhe. Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. James Kinyasi Millya, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Aidha, mapokezi hayo yanaashiria mwanzo wa utekelezaji wa majukumu yao rasmi katika nafasi zao mpya kufuatia mabadiliko ya muundo wa Serikali yaliyopelekea kutenganishwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuunda Wizara mbili tofauti, ambazo ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kuratibu na kusimamia mahusiano ya kidiplomasia ya Tanzania na mataifa mengine pamoja na mashirika ya kimataifa, wakati Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki itakuwa na jukumu la kuratibu na kusimamia masuala ya ushirikiano wa kikanda, hususan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Hatua hiyo inalenga kuongeza ufanisi katika usimamizi wa masuala ya diplomasia na ushirikiano wa kikanda pamoja na kuipa kipaumbele ajenda ya utangamano wa Afrika Mashariki.








No comments:

WAZIRI KOMBO NA WAZIRI KAIRUKI WAPOKELEWA RASMI WIZARANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashari...